UJENZI WA KISASA SOKO NA STENDI KUGHARIMU ZAIDI YA BILIONI 23 BUKOMBE

 


Na, Ernest Magashi

Ujenzi wa soko kuu na stendi ya mabasi kuanza kujengwa miundombinu za kisasa miradi hiyo miwili itagharimu zaidi ya sh 23 bilioni mjini Ushirombo makao makuu ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano Mwalwiba kwenye hafla fupi ya kufunga mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa miradi hiyo miwili na kampuni ya "China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation Co. Ltd. (CJIC)". 
Mwalwiba amesema ujenzi wa soko kuu na mzunguko wake wa vibanda itatumika zaidi sh 15.5 bilioni huku stendi ya mabasi ya kisasa ujenzi utagharimu zaidi ya sh 6.2 bilioni. 


"Tunategemea kuwa na soko kubwa sana tena la kisasa litakalokuwa na maeneo maalumu ya Mama lishe, na Baba lishe, Ofisi za Madini, Wauza Samaki, kutakuwa na vibanda 500 tofauti na vibanda vilivyopo sasa 266", amesema Mwalwiba. 

" Ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ya kisasa zimekuja fedha nyingi ambazo zimeelekezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, gharama hizi atalipwa mkandarasi mkuu,  huku mwandisi mshauri ambae atasimamia kazi nzima atalipwa zaidi ya sh 846 millioni ,"amesema Mwalwiba.

Mwalwiba ameogeza kuwa mkataba huo umefungwa Mach 14, 2025 mkandarasi anatakiwa kukabidhi mradi huo ukiwa umekamirika kila kitu Novemba 15, 2028 licha ya kutekelezwa kwa miaka miwili. 

Mkurugenzi Mtendaji Mwalwiba amewatoa hofu wamiliki wa vibanda na wafanyabiashara wanaozunguka soko hilo kuwa baada ya mradi kukamilika wao watakuwa kipaumbele wakwanza kupewa vibanda kabla ya watu wengine  kupewa. 

"tutakaa na wamiliki wa vibanda hivikalibuni  na kufanya mkutano wa hadhara ili kueleza umma utekelezaji wa mradi na faida yake", amesema Mwalwiba.

Mwalwiba ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaozunguka soko kuu kwenda maeneo yaliyo tengwa, aliyataja maeneo yaliyo tengwa soko la zamani, Kilimahewa, na Katente kwa muda ili kupisha ujenzi. 

Mchugaji Judith Shila na mwenyekiti wa Baraza la wazee Wilaya ya Bukombe Rajabu Rwezahura waliaza kwa Kumshukuru Mungu, na Serikali kwa kuleta fedha za mradi huo Rwezahura amesema kazizake hufanyia stendi ya mabasi kabla ya mradi huu alikuwa anakutana na maswali mengi itajengwa lini, sasa atatembea kifua mbele stendi kujengwa. 
Mwenyekiti wa tiba asili wilaya ya Bukombe Mohamed Hames amempongeza Rais Dkt. Samia na Mbunge wa jimbo la Bukombe na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko kwa kuendelea kuitegeneza Wilaya ya Bukombe. 


Amesema awali watu hawakuamini walizani siasa na mimi niliwaminisha mradi utajengwa na kwa hatua ya leo imejieleza tumeshuhudia utiaji wa saini kati ya halmashauri na mkandarasi ujenzi wa miradi hiyo. 

"nampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kwa kilealicho kisema Halmashauri itaendelea kuwatambua wamiliki wa vibanda hicho kilikuwa kinanipa mashaka ila kwa kilealicho kisema Mkurugenzi mtendaji tutakuwa mabalozi kusema ukweli watakavyo nufaika. 

Mhakiki wa Ujenzi Prosper Mtui alianza kwa kuishukuru halmashauri kwa kuwaamini kampuni yao kujenga mradi huo wa kujenga Soko na Stendi nakwamba viongozi na wananchi wasiwe na wasiwasi watajenga katika viwango kwa kuzingatia mkataba kwa mda uliopangwa. 

Mkandaras wa Mradi huo Peng Chao amesema mradi huo utatekelezwa hakuna Matata kama alivyo sema mhakiki wa ujenzi. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Yusuph Mohamed amesema mradi huu ambao leo tumeusaini ni Mradi Mkubwa unafedha nyingi zaidi ya sh 23 bilioni hivyo wananchi aliwaomba kuupokea vizuri na kuhakikisha mradi unafanyika nakuachana na maneno waliyokuwa wanasema baazi ya watu. 

Mohamed amesema mradi huu nimapinduzi makubwa ya kimaendeleo ikiwa stendi kuu ili kuwa haina mandhari mazuri ilikiwa ikinyesha mvua inajaa matope na soko kuu lilikuwa ni soko la kawaida lilikuwa halivutii leo linajengwa soko la kisasa, na hayo yote yanafanywa na Rais Dkt. Samia na Mbunge wetu amekuwa akichukua maadhimio ya Baraza la madiwani na kupeleka juu tunampongeza sana Dkt. Biteko. 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wanasheria wa halmashauri baazi ya wakuu wa idara na vitengo, madiwani na wazee maarufu na viongozi wa madhehebu ya dini kuona uwekwaji wa saini kwenye mikataba ya miradi ya ujenzi wa soko na stend.


 
 
 
 
 

Comments