Geita. Jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia watu wa tatu wakidaiwa kumuua baba yao mzazi Hussen Bundala mwenye umri wa miaka 103.
Ameyasema hayo kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Geita Sofia Jongo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake.
Kamanda Jongo amewataja wanaoshikiliwa na jeshi la polisi,Yombo Hussein Bundala (75) Makame Hussein Bundala (53) Shija Hussein Bundala (30).
Amesema tukio hilo lilitokea majira ya saw 2:00 usiku nyumbani kwa mzee huyo kitongiji cha Ihanamilo kata ya Nyamtukuza Wilaya ya Nyagh'wale mkoani hapa kwa kumkata nakitu chenye ncha kali kichwani.
Kanda Jongo alisema uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa kwa kushirikiana na vyombo vya dola lengo kila aliye husika namauaji hayo nikuhakikisha anakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
Comments
Post a Comment