WAFANYABIASHARA WA MBOGA MBOGA SOKO LA MAKILIKILI WAIPONGEZA SERIKALI

Na, Ernest Magashi, Geita

Geita, Wafanyabiashara wa mboga mboga solo la Makilikili eneo la CCM katoro Wilaya Geita Mkoani Geita,wameishukuru Serikali kwa kuwapa eneo hilo kwa ajili ya kufanyia biashara jioni hali ambayo inawafanya kuwa na mzunguko mzuri wa ki biashara. 
Shukurani hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na wajasiliamali wadogo wadogo wakati wakizungumza na Bukombe sasablog sokoni hapo.

Mjasiliamali wa mboga mboga soko la Makilikili Berita Sospiter alisema Serikali imefanya vizuri kwa kuwapa eneo hilo kilasiku anapata faida ambayo inamsaidi kuendesha familia. 

Berita alisema kazi hiyo ameifanya miaka miwili na miezi Sita akinunua mzigo wa sh 60,000 anapata faida ya sh 6000 hadi sh 7000 kwa siku.
Amesema biashara ya mboga mboga licha ya kuendesha familia imekuwa ikimsaidia kununua vifaa vya wanafunzi. 

Upandewake Rehema Japhet akiipongeza Serikali alisema biashara hiyo ya mboga mboga imekuwa ikimsaidia kusaidizana na baba wa familia kukuza uchumi wa familia ikiwemo kununua vifaa vya wanafunzi yakiwemo madafutari na karamu. 
"Kaziyangu hii ya kuuza mboga mboga imekuwa inanisaidia hasa baba wa familia anapokuwa amekwama au ameeda safari kupitia mboga mboga fainda nanunua vifaa vya wanafunzi nafaida nyingine natunza ili kukuza uchimi wa familia. 

Naye kijana mdogo Alex Frenki anaejihusisha na ujasiliamali wa kununua na kuuza mifuko raini  kwenye soko hilo alisema kwa siku anapata faida ya sh 10000 mtaji wa mifuko 50.

Frenk alisema asubuhi ameku anaenda shule ila jioni anaeda kujitafutia riziki ili mahitaji mengine ya shule ananunua mwenyewe na sio kilakitu wazazi au walezi.
 

Comments