Geita. Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemfagiria na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe, Dkt. Doto Biteko kwa kuendelea kupambana kuleta maendeleo jimboni.
Aliyasemahayo baada ya kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Ukumbi wa mikutano na sherehe katika shule ya sekondari Bulangwa.
Rais mstafu Dkt. Kikwete amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Bukombe kwa kuendelea kushirikiana vizuri na Mbunge na Serikali na wananchi wa kata ya Bulangwa wamejegewa ukumbi mzuri na wa kisasa utakaotumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.
Akieleza kuhusu ukumbi huo, Rais mstafu Dkt. Kikwete alisema kuwa Dkt. Biteko alifurahishwa na ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugoba uliopo katika Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani ambao ulijengwa na Kampuni na MMsteel hivyo aliomba nizungumze na Kampuni hiyo nilifanya hivyo na baadae ujenzi wa ukumbi wa Bulangwa ulianza kutokana na kijana Dkt. Biteko nampenda.
“ Niwapongeze sana wananchi wa Bulangwa kwa kupata ukumbi mkubwa na wa kisasa kutokana na kwamba haujakamilika nikipata nafasi nitakuja tena kutembelea ukumbi huu,” alisema Rais Kikwete.
Rais mstafu Dkt. Kikwete amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha na kuendeleza sekta ya elimu nchini imeboresha mazingira ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Rais Kikwete kwa kushiriki tukio hilo ambalo linaambatana na Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Bukombe unaolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Bukombe kuanzia mwaka 2020 - 2025.
Dkt. Biteko ametaja sababu ya kujenga ukumbi huo nikutokana na uhitaji kufatia uwepo wa Shule ya Sekondari Bulangwa na Chuo cha VETA kinachoendelea kujengwa sambamba na uwepo wa taasisi mbalimbali za Serikali karibu na eneo hilo.
“ mheshimiwa Rais mstafu Dkt. Kikwete Tunakushukuru sana kwa kutusaidia kujenga ukumbi wa kisasa na tunakuomba siku moja uje kututembelea wakati ukumbi huu ukiwa umekamilika,” alisema Dkt. Biteko.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bulangwa, Sane Machembe akisoma taarifa ya mradi huo alisema kuwa ujenzi wa ukumbi ulianza Mei 5, 2024 na unatarajiwa kukamilika Machi 30, 2025.
“ Ukumbi huu una uwezo wa kubeba watu 3,500 hadi 4,000 kwa wakati mmoja na utakuwa na manufaa makubwa kwa Shule hii na jamii mfano wanafunzi kuwa na sehemu nzuri na salama ya kukusanyika kwa pamoja wakati wowote na shule itaingeza kipato cha kiuchumi kwa kukodisha ukumbu,” alieleza Mkuu huyo.
Comments
Post a Comment