MBUNGE KANYASU AKABIDHI PIKIPIKI GPC

Na, m wandishi wetu Geita

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Geita Press Club (GPC) imeazieha mradi wa pikipiki ambazo zitaigiza fedha kilasiku hukuwa wanachama wakiendelea kutimiza wajibu wao kuhabarisha umma na kushiriki huduma za kiuchumi kupitia miradi ya kiuchumi katika jamii. 

Hayo  yamelezwa na katibu mtendaji msaidizi wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Geita Ernest Magashi wakati  wa makabidhiano ya pikipiki tatu ambazo zimenunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo la geita. 
Magashi alisema waliomba kiasi cha sh 10 million kutoka Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Geita Mjini kupitia mfuko wa jimbo, na amekiri kuwa GPC ilipokea kiasi cha sh 7.5 millioni fedha ambayo kamati tendaji ya GPC iliridhia zinunuliwe pikipiki tatu aina ya SanLG zenye thamani ya shilingi milioni sita na laki tisa. 


“Tuliomba million kumi kutoka Ofisi ya Mbunge kwaajili ya ununuzi wa pikipiki moja na guta, lakini tulipokea kiasi cha shilingi milioni saba na laki tano ambapo kamati tendaji iliridhia kununua pikipiki tatu badala ya pikipiki moja na guta, na hii ni kutokana na fedha kutokutosheleza kununua pikipiki moja na guta moja kama ilivyokuwa imekusudiwa”, Naibu katibu Mkuu Magashi. 
Awali kabla ya kukabidhi pikipiki hizo, Mbunge wa jimbo la Geita mjini Costantine Kanyasu alosema hatua hiyo ni kuunga mkono waandishi wa habari kwa kutambua nafasi yao katika jamii.


“Vyombo vya habari ni muhimili wa nne nchini kati ya mihimili mine nchini ambayo ni serikali kuu, Mahakama na Bunge, hivyo kukosekana kwa waandishi wa habari ni sawa na kukosa jicho," alisema Mbunge Kansas. 

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoni Geita Renatus Masuguliko alishukuru ofisi ya Mbunge kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari hasa vilivyopo GPC, na kueleza kuwa pikipiki hizo zitasaidia katika kurahisisha shughuli za kiutendaji na kujikwamua kiuchumi na kutokuwa tegemezi.

Wadau wa habari mkoani Geita Ivan Bwoya na Costantine Kalala walisema Mbunge amefanya kitu kizuri Sana ambacho kinasitaili kuingea ili wandishi wa habari ambao wako kwenye chama ambacho kinatambulika kisheria waendele kunufaika ki uchumi
Walisema kuelekea uchaguzi mkuu wanaamini waandishi wa habari ni chachu ya kutoa elimu katika kuwajengea uelewa wananchi.

 

Comments