KATA 17 KUNUFAIKA NA MIRADI YA SH 630 MILIONI ZA TASAFU MBOGWE

 

Na, Ernest Magashi


Mbogwe, kata 17 halimashari ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, kunufaika na mradi wa sh 630 milioni kuchimba na kujenga majosho kila kata kwa ajili ya kuongesha mifungo kwa wafungaji ili kuongesha dawa migugoyao na kukinga na kutibu maginjwa kwenye mifungo.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Tasafu Wilaya ya Mbogwe Revucatus Kamala kwenye Baraza la Madiwani wakati wakujadiri miradi ya maendeleo inayo tekekezwa na inayotarajiwa kutekelezwa na halmashauri. 

"Waheshimiwa madiwani kilakitu kikosawa na swala hili tunatarajia kulipeleka kwenye kamati ya fedha na mipango ili wabariki tuipeleke makao makuu ya TASAF, Taifa ili waweze kuingiza fedha sh 630 milioni na kuanza utekelezaji wa miradi kila kata itapata josho", alisema Kamala. 

Kamala aliwaomba madiwani kuwashirikisha wananchi ujio wa mradi huo pia wananchi wawetayari ku upokea ili wanufaike kwa pamoja wakiwemo wafungaji. 

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Mbogwe Josephat Chacha amesema halmashauri ihakikishe inatekeleza miradi yote ambayo iko kwenye mpango na ambayo inakuja ili kuwaletea maendeleo wananchi. 

Chacha aliongeza kuwa niwakati wa kuongeza kasi ya utendaji ili wananchi waendele kufrahia Serikali yao ya CCM. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbogwe Vicent Businga alikuhakikishia Mratibu wa TASAF Wilaya watabariki na kupitisha haraka ili fedha zije mapema. 

Businga aliwapongeza watalamu wa halmashauri yake kwa jitihada wanazofanya kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hali ambayo inachagia kukuza uchumi kwa wananchi.



Comments