JESHI LA POLISI GEITA LIMEKIRI KUMKAMATA KIONGOZI WA NETO

Na, Ernest Magashi

Geita. Jeshi la polisi mkoa wa Geita limekiri kumkamata kiongozi wa kundi sogozi la WhatsApp  la umoja wa waalimu wasio na ajira nchini  (NETO) mkoa wa Geita Joseph Paulo (31) uchunguzi wa awali unafanyika

Kiongozi huyo alikamatwa Februari 24 mwaka huu 2025 na taarifa za kukamatwa kwake zikitolewa na uongozi wa NETO pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Safia Jongo alisema baada ya mahojiano na uchunguzi wa awali wamebaini kuwa umoja huo hauna usajili kutoka mamlaka za kisheria na mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi unaendelea. 

Kamanda Jongo hata hivyo jeshi la polisi Mkoa wa Geita limesema halitavumilia uwepo wa makundi ya uvunjifu wa amani, hivyo kila mmoja anao wajibu wa kujiepusha na makundi hayo kwani atakayebainika atachukuliwa hatua na vyombo vya dola.

Comments