Na, Ernest Magashi
Mbogwe. Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, Sakina Mohamed amewaagiza watalamu na madiwani kuwana ushirikiano na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kufikia malengo ya halmashauri.
Aliyasema kwenye Baraza la madiwani baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sada Mwaruka kuaga kwenye halmashauri hiyo kufatia mhe, Rais Samia Suluhu Hasan kuteua na wengine kusubiri kupangiwa kazi zingine.
"Nampongeza sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazofanya za kuleta maendeleo kwenye taifa huku akifanya mabadiliko ya wateule wake Mbogwe tumepokea Katibu tawala, na Mkurugenzi mtendaji mpya licha yakwamba munaodoka ila tutawakumbuka tulivyo fanya kazi vizuri namumechagia sehemu kubwa ya kupandisha mapato ya ndani ya Halmashauri", alisema Sakina.
"Nawaombeni sana Mkurugenzi na Katibu tawala ambao mueletwa Mbogwe tushirikiane ili halmashauri na Wilaya ifikie malengo ya Serikali na kukamirisha miradi vipolo ili Madiwani waende kuelezea kwa wananchi wafanikio ya Serikali", alisema Sakina.
"mpaka anaondolewa kwenye nafasihiyo na kusubiri kupangiwa kazi nyingine na Mhe, Rais Samia halmashauri ya Mbogwe inakusanya sh 3.2 bilioni mapato ya ndani na sh 500 milioni zimetolewa kwenye vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu", alisema Pili.
Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga aliaza kwa kimpongeza Mkurugenzi aliyemaliza mdawake kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kubuni vyanzo vya mapato na kipandishi mapato ya halmashauri.
Maganga aliwaomba walioteuliwa na Rais Samia na kipagiwa Mbogwe wafanyekazi kwa upendo na kuyaendeleza walipoishia waliotoka na kwamba ofisi yake itatoa ushirikiano kwa watalamu ili kufikia malengo ya kimaendeleo.
Mkurugenzi mtendaji aliyemaliza mdawake Sada Mwaruka akiwaaga madiwani na watumishi aliwashukuru wananchi madiwani na watalamu wa halmashauri ya Mbogwe kwa ushirikiano waliompa na kufikia hapo alipoishia.
Akiwaaga madiwani na watumishi Jacob aliwashukuru kwa ushirikiano ambao wamempatia katika utendaji kazi wake na kwamba atawakumbuka DE-D anaeondoka na DC anaeendelea kuwatumikia wananchi wa Mbogwe.
Rombo aliwaomba kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano na kuacha kufanyakazi kwa kuchukiana na badalayake upendo utawale.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe Edwin Lusa aliaza kwa kumushukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbogwe nikotayari kutumika na kupokea ushauri aliomba Baraza la madiwani kuendeleza ushirikiano.
Lusa alimpongeza Mkurugenzi mtendaji wa zamani kwa kazi aliyoifanya na kwamba Mungu aendele kumlinda wakati akisubiri Mhe, Rais Samia kimpagia majukumu Mengine.
Katibu tawala Wilaya ya Mbogwe Paul Faty akimshukuru Mhe, Rais Samia kwa kumteua kuja kuwatumikia wananchi kupitia Baraza hilo alimpongeza DE-D aliyemaliza mdawake na DAS aliyehamishwa kwa kazi nzuri waliyoifanya na kwamba amefika Mbogwe amekutana na wanafunzi wake aliowafudisha chuo.
Comments
Post a Comment