Na, Ernest Magashi
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mkoani Geita Dkt. Doto Biteko ameongoza shughuli za kuaga na kukabidhi ubani kwa wafiwa huku akiwataka kuwa wavumilivu hasa kipindi hiki cha majonzi.Dkt. Biteko leo Januari 30, 2025 mkoani Geita, maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya wanafunzi saba wa Shule ya Sekondari Businda iliyopo kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe waliofariki kwa kupigwa na radi Januari 27, 2025.
Dkt. Biteko ametoa pole kwa wazazi, walezi ndugu wa watoto pamoja na wanafunzi wa Businda kwa kuondokewa na wapendwa wao na wanajamii wa Businda Sekondari kwa jitihada na utoaji wa huduma wakati wa tukio hilo.
“ Imeandikwa kwamba shukuruni Mungu kwa kila jambo, Mungu ametukutanisha leo katika hali ya majonzi. Tukio hili litukumbushe kutenda mema wakati wote na tuamini kwamba Mungu ndiye mwenye uweza. Kipekee ningetamani kuwataja Madaktari wote kwa majina katika hospitali ya Wilaya na San Pio kutokana na msaada mkubwa walioutoa lakini itoshe kusema asante
kwa kazi kubwa mliyoifanya” amesema Dkt. Biteko.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea taarifa za msiba huo mzito amekuwa akifuatilia kwa karibu na kutoa maelekezo kwa ajili ya kuzifariji familia za wafiwa, wana Bukombe na Taifa kufuatia kuondokewa na vijana waliokuwa katika safari ya kutafuta elimu.
“Rais Samia amegharamia msiba pamoja na kutoa ubani kwa kila familia za wafiwa pamoja na kugharamia usafirishaji wa miili ya wanafunzi wawili kwenda Chato, Geita na Karatu mkoani Arusha kwa mazishi",amesema Dkt. Biteko.
Viongozi mbalimbali wa dini wamewapa faraja wafiwa na kusema msiba haujawahi kuzoeleka lakini kwa mapenzi ya Mungu atakuwa mfariji wao.
Viongozi hao wamewataka wanadamu kujipanga wakati wote kwa kuwa hawajui ni wakati gani utafikwa na umauti kutokana na fumbo aliloliweka Mwenyezi Mungu, wamemwomba Mungu awape uvumilivu viongozi katika kipindi hiki cha majonzi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Businda, Theodora Mushi amesema wanafunzi hao walipatwa na umauti wakiwa katika harakati za kusaka elimu.
Wanafunzi wanne kati yao walifariki papo hapo na wengine watatu walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali na vituo mbalimbali vya Afya.
Mshi aliwataja waliofariki ni Erick Martin Bugalama (18) Erick Emmanuel Akonai(18), Nikas Paul Tompoli (17) Peter Nkinga Manyanda (18) Gabriel Daud Makoye (17), Esteria Leonard Mkuna (16) Doto Marko Masasi (17) wote kidato cha tatu.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mhadis Paskas Mragili akitoa shukuruni idara ya afya kwa uharaka wa utoaji huduma kwa wanafunzi baada ya tukio majira ya saa 8:20 mchana Januari 27,2025 wakiwa darasani.
Mhadis Mragili amesema kidato cha tatu darasa lilikuwa na wanafunzi 138 ambapo wanafunzi 89 walipigwa na radi katiyao saba walipoteza maisha huku 82 waneruhusiwa kutoka hosipitalini.
Kwaniaba ya wafiwa Daud Makoye ambaye nimtumishi wa halmashauri ya Wilaya Mbogwe akitoashukuruni kwa Serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuokoa maisha ya wanafunzi, licha ya wengine saba kupoteza maishi akiwemo mwanangu.
"Kwaniaba ya wafiwa wezagu nimesimama hapa kuishukuru Serikali hasa Serikali ya Wilaya ya Bukombe ambayo nao nishehemu ya wahanga wa tukio hili nikweli kwamba sisi wazazi, walezi wa watoto hao ambao leo tunawaona kwenye masanduku tulitamani sana tuendelee kuwanao leo wametangulia mbele ya haki nawaombeni wanafunzi walioachwa endeleeni kusoma msikate tama", alisema Baba mzazi wa Gabriel Makoye.
Dhaaaaaaaaaaa mungu awe nanyi katika hiki kipindi kigumu ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
ReplyDeleteInasikitisha sana ila Mungu nimwema Kila wakati.. EEEh mwenyez Mungu mwing wa rehema wajalie faraja Hawa wazazi walio ondokewa na familia zao Amina
ReplyDelete