WANAFUNZI SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA NA RADI WENGINE 82 WAKIJERUHIWA

Na, Ernest Magashi 

Wanafunzi 89 wamepigwa na radi saba wakifariki dunia na wengine 82 kujeruhiwa wakiwa darasani kidato cha tatu shule ya Sekondari Businda iliyopo kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhadis Paskas Mlagili amedhibitisha tukio hilo akiwa hospitali ya Wilaya baada ya kupokea taarifa ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dkt. Deograsia Mkapa alipo tembelea hospitali kuonamajeruhi na kuona wanafunzi waliofariki.
Mlagili amesema tukio hilo limetokea nalimeleta mshituko kwa wananchi akiwaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu kwa wakati huu mugumu amesema tukio hilo lilitokea wakati mvua ikinyesha iliyokuwa imeabatana na radi huku wanafunzi hao wakiendelea na masomo darasani. 

Amesema madaktari kwa kushirikiana na watalamu wa afya hospitali ya Wilaya wanaendelea kutoa huduma na baazi majeruhi wa naendelea vizuri lakini Mkoa watafika hospitalini hapa kuongeza nguvu za kitabibu. 
Amesema Serikali itaendelea kutoa taarifa ya kinachoendelea na kwamba mazishi ya wanafunzi waliofariki dunia yataghalimiwa na Serikali yakiwemo matibabu na wananchi wamefika hospitali wakiwemo wazazi kujua taratibu za Serikali ambapo Serikali imelibeba. 

Diwani wa kata ya Ushirombo Lameck Warangi amesema tukio hilo limetokea Januari 25, 2025 majira ya saa 8:30 mchana wakati mvua ikiendelea kunyesha. 

Warangi amesema wananchi wamepata mshituko na kwamba Serikali imesaidia Sana kwa kuwachukua wanafunzi shuleni na kuwakimbiza hospitali ya Wilaya kwa kitumia magari ya kubeba wagonjwa huku polisi wakiwa wamefika eneo la tukio. 

Mkazi wa Kata ya Bulangwa Sada Ramadhani ameishukuru Serikali kwa huduma ambayo imetoa kwa majeruhi locha ya tukio hili la Radi limeshitua wananchi kutokana na tukio hilo kuwa la kwanza wanafunzi kupigwa radi wakiwa darasani.

Miongoni mwa wanafunzi majeruhi Edina Sitta amesema wali kuwa darasani gala waliona kama giza huku akasikia wezake wanapiga kelele hakujua kilicho endelea amekuja kupata fahamu hospitali ya Wilaya.
Mwanafunzi huyo ameishukuru Serikali kwa huduma ambayo wanaedelea kupata katika hospitali ya Wilaya anaomba Mungu awaponye. 
 

Comments