Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Geita, Pili Ndimila amewataka wanawake wa wilaya ya Bukombe kuhakikisha Dkt. Biteko anapita bila kupingwa uchaguzi ujao 2025.
Pili alitoa wito jana Januari 7, 2925 aliposhiriki kikao cha baraza la wanawake wilaya ya Bukombe na kutoa semina kwa wenyeviti, makatibu kutoka kata 17 pamoja na madiwani wanawake kwenye ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo.
“Tunajua chama chetu kinaruhusu kila mtu kuomba uongozi ila kwa Bukombe tusingependa kuona mtu anajitokeza kugombea kutokana na kazi nzuri anayoifanya Dkt. Biteko katika wilaya hii” alisema Katibu Pili
Alifafanua kuwa, kwa upande wa Rais Samia na Dkt. Biteko stahiki yao ni kupata kura za kishindo ikiwa ni shukurani kwa hatua ya maendeleo inayoshuhudiwa jimboni humo.“Sisi UWT hatuna mashaka kutangaza hadharani kwamba tuna mgombea mmoja wilaya ya Bukombe. Kwa heshima tuliyopewa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutupatia Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu” alisema Pili.
Katika ziara hiyo ya kikazi aliyoianza jana wilayani Chato ambapo alifanya semina kwa mabaraza ya wanawake, makatibu muhtasi (personal secretary- PS) na madiwani wanawake, amesema lengo lake ni kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM kwa kuimarisha umoja kuelekea uchaguzi huu wa 2025.
“Ziara yangu nikuwakumbusha tu, kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na sisi wanawake ambao ndiyo wabeba MAONO twendeni tukahamasishe wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani Rais Samia tayari ameonesha mfano bora kwa uongozi mzuri katika ya juu ya uongozi“ Alifafanua Pili Ndimila- Katibu wa mkoa, UWT akiwasihi wanawake kutojiona wanyonge kwakuwa wanaweza.
Aidha, aliongeza kuwa wilaya Bukombe kwa kuongoza katika matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ikiwemo vijiji viwili na vitongoji 13 kunyakuliwa na wanawake ikiwa ni mara ya kwanza kupata mafanikio hayo.Kadhalika, alimpongeza Mbunge wa jimbo la Bukombe, Dkt. Biteko kwa kazi aliyoifanya kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Geita kunadi wagombea wa CCM jambo lililochangia kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo katika mkoa wa Geita.
“Mimi kama katibu wa UWT mkoa wa Geita, kwaniaba ya chama nimekuja kumshukuru Dkt. Biteko kwa kazi aliyoifanya katika wilaya zote za mkoa huu” ameshuru, Pili kwa niaba ya UWT akieleza kuridhishwa jinsi mbunge huyo anavyosimamia maendeleo ya wilaya ya Bukombe na kutoa rai kwa wenyeviti na makatibu wa UWT kata kushuka hadi kwenye matawi kuwashukuru wananchi kwa kufanya vizuri katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa.
H
ata hivyo, pamoja na kushukuru amewataka viongozi hao waombe tena kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 utakaohusisha madiwani, wabunge na Rais.
Comments
Post a Comment