UBORESHAJI MIUNDOMBINU ILIYOCHAKA UTAMALIZA CHANGAMOTO ZA UMEME-DKT BITEKO

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko Amesisitiza umuhimu wa kuboresha Miundombinu ya ya usafirishqji umeme, akieleza kwamba njia nyingi za kusafirisha umeme zimekuwa za zamani na zimezidiwa na mahitaji makubwa ua wananchi.


"Kwa mfano katika Jiji la Dar es Salam tumepnga kuongeza uwezo wa kinyerezi kwa MVA 75,Gongo la mboto kwa taransofa ya 120 MVAz na mbagala kwa kuongeza 120 MVA. Lengo letu ni kuboresha usambazaji wa umeme kutoka kinyerezi hadi gongo la mboto,mbshala,na baadae kuunganisha Dege na Mkuranga" Amesema Dkt abiteko.


Dkt Doto Biteko ameongeza kuwa baada ya Marekebisho hayo changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme ikiwemo kukatika kwa umeme zitapungua na hali ya umeme itaweza kuwa endelevu


Umeme hautaki maneno, upo utaouona haupo hautouona amesisitiza Dkt Biteko akionyesha matumaini ya namna serikali inavyopambana kumaliza changamoto ya umeme nchini.

Comments