NISHATI YA UHAKIKA INAKUZA UCHUMI WA NCHI - DKT. BITEKO

 



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Januari 10, 2025 amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unategemea upatikanaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu.

"Kwa nchi yoyote inayotaka kukua kwa kiasi kikubwa inategemea Nishati inayopatikana kwa hakika na yenye bei nafuu, Bila nishati ya gharama nafuu, uchumi utabadilika na bidhaa zitazalishwa kwa gharama kubwa zaidi," amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko amesisitiza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa gharama nafuu ili kuchochea Maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.


Comments