HATUA KUBWA IMEFIKIWA UZALISHAJI UMEME BWAWA LA JULIUS NYERERE - DKT BITEKO

 

Dkt Doto Biteko, Amesema kwamba hatua kubwa imefikiwa katika miradi ya kuzalisha umeme wa bwawa la Julius Nyerere, akibainisha kuwa mitambo sita tayari imeshawashwa, na mitambo mitatu iliyobaki inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili.


"Tumefanikiwa kuwasha mitambo sita, na bado mitambo mitatu ilikukamilisha jumla ya mitambo tisa. Tunaamini ndani ya miezi Miwili tutakuwa tumekamilisha kazi hii, Tumepiga hatua nzuri" Amsema Dkt biteko.


Mradi wa bwawa la Julius Nyerere unatarajiwa kuwa moja ya Miradi mkubwa zaidi ya nishati barani africa, Mradi huo ukilenga upatikanaji wa umeme wa uhakika na gharama nafuu kwa Watanzania.


Ametoa kauli hiyo leo Januari 10,2025 wakati wa mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa TBC1

Comments