Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda sekondari kwa masikitiko makubwa.
Naomba kuwapa pole sana wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa shule ya sekondari Businda na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa.
Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote.
Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu.
Aidha tunawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote kwenye kadhia hii.
Nimemuomba Mhe. wa wilaya, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya Majeruhi wote na taratibu za mazishi ya watoto wetu wapendwa waliotangulia mbele ya Haki.
Doto Biteko(Mb),
Jimbo la Bukombe
Comments
Post a Comment