JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUKAMATA SHEHENA NYINGINE KUBWA YA NYAYA ZA SHABA MALI YA TANESCO PAMOJA MA TRC



Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rujifi limewakamata Watu wawili ambapo mtu mmoja akiwa na asili ya Kiasia na mwingine akiwa ni Mtanzania kwa tuhuma za kukutwa na shehena ya nyaya za shaba mali zilizoibwa katika Miundombinu ya Umeme - TANESCO na Shirika la Reli Tanzania (TRC). 




Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi imeeleza kuwa Watuhumiwa hao walikutwa na copper block 426 zenye uzito wa kilogramu 7,728 na Cooper Wire zenye uzito wa kilogramu 2628.5 ambazo ni mali za TANESCO zilizoibwa pamoja na Waya za Copper za TRC zenye uzito wa kilogramu 430.


Chanzo cha kukamatwa kwa Watuhumiwa hao ni baada ya kukamatwa gari aina ya Fuso lililokuwa likisafirisha Nyaya hizo kutoka kiwanda chao kwenda kuzificha kutokana na masako mkali wa jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani humo.


Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rujifi limetoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano katika kubaini, kuzuia na kuwakamata wale ambao hawataki kufuata njia halali za kujipatia kipato na badala yake wanahujumu miundombinu ya Serikali.

Comments