Na, Ernest Magashi
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Geita kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura kesho na kuchagua wagombea wa CCM.A
mewahimiza wananchi hao kuendelea kumuunga mkono yeye na CCM ili kutoa fursa ya kuendeleza jitihada za maendeleo “Nimekuja hapa kuwaambia msiniangushe wala kuiangusha CCM kwa kuwa miradi na juhudi zote zinazoendelea zinalenga kuleta maendeleo kwenu,”
Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 26, 2024 wakati akihutubia kwenye mkutano wa ahadhara wakufunga Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mkoa wa Geita zilizofanyika katika Uwanja wa Mwenge kata ya Uyovu, Wilaya ya Bukombe mkoani hapa.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa kampeni za 2024 zimekuwa za kistaarabu huku akiwashukuru wanachama wa CCM kwa kuendeleza kauli mbiu ya Rais Samia ya kujenga Taifa moja la kuheshimiana na kustahimiliana.
Dkt. Biteko alitaja sababu za kuwaomba wananchi hao kuipigia kura CCM kuwa “Wana Uyovu nataka niwakumbushe kazi ambazo zimefanywa tangu mwaka 2015, Kata hii ya Uyovu ilikuwa na shule za msingi tano, tumejenga 7 sasa zipo 12, zilikuwa shule za sekondari mbili, tumejenga zingine ili ziwe sita,” amesema.
Arifafanua kwa kusema Serikali inayoongozwa na CCM imeimarisha miradi ya maji, imejenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.2 na pia katika Wilaya ya Bukombe kinajengwa Chuo cha VETA.
Dkt. Biteko amesema vyama vya upinzani si vibaya, watu washindane kwa hoja na sio kubaguana huku akiwataka wagombea wa CCM watakapochaguliwa wafanyekazi kwa uaminifu na uwazi ili kuchochea maendeleo kwa wananchi.
“ Tunataka uchaguzi huu uwe wa amani, wa kistaarabu na wa haki kusiwe na kubebwa, uchaguzi huu usitufanye tugawanyike, ufanyike kwa amani na utufanye tuwe wamoja na baada ya uchaguzi tuijenge wilaya yetu, siasa ziwe daraja la kutuunganisha na kushindanisha mawazo,” aliongeza Dkt. Biteko.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Nicholous Kasendamila na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Alexandrina Katambi kwa nyakati tofauti wamewataka wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura kesho na kuchagua wagombea wa CCM.
Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Bukombe, Matondo Lutonja amewashukuru wananchi wa Geita kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa ufungaji kampeni na kuwaomba mitaa, Vijiji na vitongoji vyote tunavitaka CCM.
Licha ya kugunga kampeni hizo kimkoa Dkt. Biteko ameshiriki mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Wilaya tano za Mkoa wa Geita ambazo ni Mbogwe, Chato, Geita, Bukombe na Nyang’hwale akihamasisha wananchi waichague CCM na Mitaa, Vijiji na Vitogoji vyote washinde wa bomber wa CCM huku wananchi wakiitikia tunachikua vyote CCM.
Mkutano huo wa ufungaji kampeni umeambatana na burudani kutoka katika vikundi vya sanaa zaidi ya 40 kutoka kata mbalimbali ndani ya Bukombe.
Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba, 20, 2024 kupitia viongozi mbalimbali wa CCM kufanya uzinduzi katika mikoa mbalimbali ambapo Dkt. Biteko alizindua Kampeni hizo mkoani wa Mara na kufunga mkoani Geita.
Comments
Post a Comment