Wananchi wa Wilaya ya Bukombe wameungana na watanzania wengine katika maeneo mbalimbali ya nchi kujitokeza kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wao ngazi ya Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji.
Hata Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko media kura ikiwa nihaki yake ya Kikatiba katika Kata ya Bulangwa, Wilayani Bukombe mkoani Geita kisha akawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Msingi Bulangwa wilayani Bukombe mkoani hapa.
“ Zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi nawapongeza kwa hilo na Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti kwa sababu ya hamasa kubwa ya kushiriki,” amesema Dkt. Biteko.
“ Ninaomba watu wote waliojiandikisha watumie haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kwa wingi na kwenda kupiga kura ili kupata viongozi bora,” aliogeza Dkt. Biteko.
Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizinduliwa Novemba 20, 2024 na kuhitimishwa Novemba 26, 2024 baada ya wagonbea kujinadi na kuomba kura kwa wananchi.
Mkazi wa Bulangwa Pili Mathias amesema leo amepiga kura kwa Mara ya kwanza baada ya kujiadikisha kwenye daftari la wapiga kura mwaka jana na leo ameona faida, kwa kuchagua kiongozi wake na ku ungana na Mbunge wake Dkt. Biteko kwenye kupiga kura.
Comments
Post a Comment