Na, Ernest Magashi Mbogwe
Madiwani wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita wametakiwa kuwanamahusiano mazuri na watalamu wanapokuwa kwenye majukumu ya kikazi ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuzingatia mipaka ili kufikia malengo ya kimaendeleo haliambayo itaodoa changamoto ya watumishi kuhama.
Wito huo ulitolewa kwenye kikao cha baraza la madiwani na katibu tawala wilaya ya Mbogwe Jacob Rombo wakati wa kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na changamoto za Upungufu wa watumishi na ukusanyaji wa mapoato ya ndani.
Jacob alisema kunabaazi ya madiwani wame kuwa chanzo cha watumishi kuomba kuhama wakati ilipaswa ku tegeneza mahusiano na walamu aliwataka kama kunamtumishi hatekelezi majukumu yake kiusahihi watoe taarifa kwa Mkurugenzi mtendaji na sio kuwaharasi na kuwafoka haliambayo inawafanya wengiwao kuhama.
Awali afisa mtendaji wa kata ya Lulembela Franck Ngory alisema Changamoto kwenye kata hiyo niupungufu wa vyumba vya madarasa shule za msingi na sekondari pia upungufu wa watumishi hasa idara ya Elimu licha ya ukusanyaji mapato hatua iko vizuri.
Diwani wa kata ya Nyasato Mariko Nzela aliliambia baraza la madiwani kuwa Upungufu wa watumishi nimkubwa kiwilaya watumishi 15 hadi 20 kila mwezi wanahama kwenda nje ya wilaya.
Nakwamba Watumishi 39 wamehama halmashauri ya Mbogwe kuanzia Julai hadi Septemba 30,2024 wengiwao wakidai wanafata wezi wao na wengine ni kwa mjibu wa kanuni za mtumishi wa umma.
Halmashauri ya Mbogwe ina uhitaji wa watumishi kuanzia Elimu Msingi 218 Elimu Sekondari 487 Afya wanatakiwa watumishi 539.
Mkurugenzi mtedaji wa halmashuari ya Mbogwe Sada Mwaluka alisema changamoto hizo amezipokea na atazifanyia kazi ikiwemo ujenzi wa machinjio kata ya Lulembela.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Vicent Businga alisema katibu tawala amesema Mambo mazuri sana kuhusu watumishi na madiwani kuwanamahusiano mazuri.
Visent alisema bazi ya watalamu wanekuwa nachangamoto ya kutojuwa kufanya walicho somea hadi kuajiliwa na Serikali haliambayo inapeleke wananchi kukosa maana ya watalamu katika uajibikaji.
Muweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Jemes Igoti akizungumzia ukusanyaji wa mapato ya ndani aliliambia baraza kuwa ukiodoa changamoto ya upungufu wa watumishi waliopo wamekuwa wakiedele kujituma katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na makusanyo ya mapato ya ndani kuanzia Julai 30 hadi Septemba 30 2024 halmashauri imeweza kukusanya sh741.9 milioni licha miezi mitatu hiyo waliyojiwekea malengo ya kukusanya sh 813.4 milioni.
Jemes aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kukusanya mapato ya ndani sh 3.2 billioni hivyo kwamikakati na malengo yao waliyo jiweke halmashauri nikufikia ukusanyaji huo ili kufikia malengo ya Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Jemes alisema pamoja na madhimio ya kikao cha baraza la madiwani kuhusu ukusanyaji wa mapato ya ndani ofisi ya mapato kwa kushirikiana na watalamu wengine chini ya usimamizi wa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri mama machachali mpambanaji Sada.
"tumeweka mikakati ya kwamba katika robo ya pili Oktomba hadi Desenba 30,2024 tutahakikisha asilimia ambayo haijakusanywa kwa robo ya kwanza inafikiwa ili kufikia malengo ya halmashauri ya kukusanya sh 3.2 billioni kwa mwaka wa fedha", alisema Muhazina huyo Jemes.
Jemes alitaja mikakati mingine waliyojiwekea ni usimamizi wa makusanyo ya mapato ya ndani na kuongeza Pos ili kila kijiji kiwe na pos na kata zote 17 ambapo kwa sasa halmashauri imegawa posi kwenye vijiji 63 na pos kwenye kata 10.
Alisema mahitahi ni pos 104 zilizo kabiziwa kwa ajili ya ukusanyaji mapato ni Pos 73 bado Pos 31 zinatarajiwa kukabiziwa kwenye vijiji na kata zilizobakia kulingana na uhitaji ikiwa halmashauri ya Mbogwe ina vijiji 87 na kata 17.
Comments
Post a Comment