Na, Ernest Magashi, Bukombe
Timu Bukombe Combine Sports Club mabigwa daraja la tatu msimu 2023/2024 imetoa kichapo cha goli 1-0 Aiport fc mabigwa wa ligi ya CRDB Federation Cup Mkoa wa Kigoma katika uwanja wa Kilimahewa wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.
Mfungaji wa goli la Bukombe Combine Sports Club Mlope Thomas dakika ya 76 hali ambayo iliwafanya mashabiki wa timu hiyo kuinuka na kushagilia huku wakisikika wakitaja KNK yaani Kusema Na Kutenda kelele hizo za mashabiki ziliendelea kusikika kwenye masikio ya watu uwanjani hadi kipenga cha mwisho.
"Mchezo umeenda vizuri kwa kweli na wapongeza wachezaji kwa kujituma na kufuata maelekezo " Alisema Benard Simon kocha Mkuu wa timu ya Bukombe Combine Sports Club.
Benard aliongeza kuwa kutokana na ushindi huo wanajiada kwa kufanya mazoezi ili kuwakabili wapinzani wao watakao pangwa.
Kocha mkuu wa timu ya Aiport fc John Joseph ameeleza kuwa mchezo ulikuwa mzuri timu yake ilifanya makosa na wamefungwa na wamepokea matokeo hayo nihalali.
John aliwatakia maandalizi manzuri kwa kuelekea mchezo wao wa pili na wapate matokeo manzuri ikiwa Bukombe Combine Sports Club ni timu ambayo ninzuri.
Comments
Post a Comment