ROSE AWATAKA WANANCHI KUMUUNGA MKONO DKT. BITEKO

 

Na, Ernest Magashi, Bukombe

Wananchi Wilaya ya Bukombe Mkoani wa Geita, wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Mbunge wa jimbo la Bukombe pia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika shughuli za miradi ya maendeleo. 

Wito huo umetolewa leo Oktoba 1,2024 na Mbunge viti maalumu Mkoa wa Geita Rose Businga wakati akizungumza kwa niaba ya Dkt. Biteko kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru mjini Ushirombo. 

Rose alisema Serikali kwa kupitia Mbunge Dkt. Biteko imekuwa ikileta fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi wake. 


Alisema licha ya kuwepo miradi mingine inayo tekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi kalibuni halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imeleta fedha  sh4.1 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 11 ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru hivi leo na hakuna mradi ulio kataliwa zote ziko vizuri. 

Rose aliwaomba wananchi kuchagua viongozi bora kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika mwaka huu 2024 ili kuwaviongozi sahihi watakao simamia maendeleo. 

Viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava alimpongeza Mbunge wa jimbo la Bukombe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Biteko kwa kazi nzuri ya miradi ya maendeleo inayo fanyika kwa ushirikiano mzuri na wananchi na viongozi wengine wa Serikali. 

Mnzava aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika miradi ya maendeleo na kufanyikazi kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024.


"Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"

Katika eneo hilo la Mkesha wa Mwenge Sophia Paul mjasiliamali wa vinywaji alisema ujio wa Mwenge nifrusa kwake na wezake ambapo mauzi leo ymeongezeka kutoka sh 40000 hadi sh 87000 na huenda ikapanda zaidi.

Comments