MWENGE WA UHURU KUPITIA MIRADI YENYE GHARAMA ZAIDI YA SH BILIONI 4.1 BUKOMBE



Na, Ernest Magashi Bukombe

Mwenge wa Uhuru Wilayani Bukombe Mkoani Geita utakimbizwa  kilomita 126 kutoka kijiji cha Nampalahala hadi eneo la mkesha na makabidhiano huku ukipitia, kukagua na kufungua miradi 11 yenye thamani ya sh 4.1 bilioni. 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mhandisi Paskasi Muragili Wakati akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Chato Louis Bura kijiji cha Nampalahala leo Oktoba 1, 2024 mjira ya saa 1:2 asubuhi. 

Mhandisi Muragili ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwenye miradi ya maendeleo itakayo pitiwa na mwenge wa Uhuru.pia aliwakaribisha  kujitokeza kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru Stend ya Mabasi mjini Ushirombo.

Alisema Kauri mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 "Tunza Mazingira Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Haifa"

Mkuu wa Wilaya ya Chato Louis Bura  akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Bura alisema Mwenge wa Uhuru  ukiwa Wilayani Chato ulikimbizwa umbali wa kilomita 145 na kupitia, kukagua na kufungua miradi 10 yenye thamani ya zaidi ya sh 10 bilioni.

Mkazi wa Nampalahala Susana Paschal (45) alisema leo ni siku yake ya kiistoria kuona Mwenge wa Uhuru alidai kuwa tangu azaliwe alikuwa hajawahi kuona Mwenge licha ya kusikia huwa unawashwa na kuzimwa na Rais kwa lengo la kuhamasisha maendeleo.


Comments