Kuelekea mbio za mwenge kufika tamati kama ilivyo kawaida mwenge wa Uhuru uzimwa Oktoba 14 kila mwaka kiongozi wa mbio za mwenge 1999 Julius Masubo Kambarage amemkumbuka Asha Mbwana aliye kimbizanae mwenge kwa sasa ni marehemu.
Kwa sasa kiongozi huyo anaitwa Mfalume Julius Masubo Kambarage kutokana na kazi za kisiasa na kijamii anazofanya ila kuelekea tamati za mbio za mwenge Oktoba 14,2024 jijini Kwanza ametumia frusa hiyo kumkumbuka sana Asha na kumuombea kwa Mungu aendele kumtunza licha ya wa Tanzania tunamkumbuka kwa alivyo jitoa kulitumika Taifa.
Mfalume Kambarage ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mara aliye wahi kukimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa licha ya kukumbuka mwezake mwaka1999 wakiendelea na mbio za Mwenge Wakati Baba wa Taifa akiugua na Hatimaye kufariki dunia Kwa Mara ya kwanza Mwenge wa Uhuru ulisimama Mwezi Mmoja.
Mfalume Kambarage akizungumza na gazeti la MAONO alisema tulikuwa tumefika Mkoani Shinyanga mjini, Nabaada ya Maziko Safari iliendelea, Wakimbiza Mwenge Wakati huo Mwenge ulikimbizwa na Vijana 4 tu!.
Ambao ni Julius Masubo Kambarage kiongozi Toka Bara, Bi Asha Mbwana Marehemu sasa, Ali Ramadhani Mwalimi Toka Kisiwani Unguja na Ali Rashi Aliy Toka kisiwani Pemba.
Kuelekea Oktoba 14 anamkumbua pia Mh. Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjani Mkapa akimkabidhi Mfalme Julius Masubo Kambarage Hati Maalumu ya Uongozi uliotukuka Baada ya kukamilisha Majukumu aliyo pewa ya Kukimbiza Mwenge nchi Nzima na wezake Bara na Visiwani 1999, Mwaka aliofariki Baba wa Taifa, Sasa ni miaka 25 imepita.
Mfalume Kambarage alisema mwaka huo kauri mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru "Mazingira ni uhai panda miti tunzaazingira na Jenga vihenge tunza Chakula Ukimwi unaua tunza Afya yako tumia condom",
Mfalme.
Mkazi wa Ushirombo Nyauke Nyauke alisema licha Kambarage kukimbiza mwenge alikuja wilayani Bukombe akiwa mtumishi wa Umma Afisa utamaduni badae alihamia Halmashauri ya Kahama akahamishiwa Jiji la Mwanza leo pia ni Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Mara.
Comments
Post a Comment