KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNZIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU BUKOMBE

 

Na, Zena Seleman Bukombe

kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amekabidhi vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 385 wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Ushirombo iliyopo wilayani Bukombe Mkoani Geita. 

Alikabidhi Vifaa hivyo wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa shuleni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa shule ya msingi Ushirombo unaotoa huduma ya kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. 

Mzava akikabidhi vifaa hivyo ni  madaftari ,kalamu cherehani , pamoja na maswetwa, licha ya vifaa hivyo kiongozi wa mbio za Mwenge alitembelea bustani ya mbogamboga zilizo pandwa na wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu kwa ajili ya lishe. 


Wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huoo mkuu wa kitengo maalumu  Elimu maalumu  Wilaya ya Bukombe Joyce Mangi alisema shule inawanafunzi 385 wavulana 192 wasichana 193, huku wenye ulemavu wa akili 116, viziwi 54, Ulemavu wa viungo 155, na wenye Ualbino  15.

Joyce alisema wanafunzi wenye mahitaji maalumu wananufaika na elimu kwa kumudu stadi zao mbalimbali za maisha na kuibua vipaji walivyonavyo. 

Joyce amemshukuru kiongozi wa mbio za kitaifa kwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu huku  akiishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa vifaa vya usaidizi kwajili ya kujifunzia wanafunzi hao.



Comments