DKT. BITEKO NA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WAHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA BUKOMBE
Ernest Magashi-Bukombe
Wananchi wilayani Bukombe Mkoani Geita wametakiwa kujiandikisha kwenye daftari la wa piga kura ili watumie Friday ya kikatiba kuchagua Viongozi kwenye Serikali za mitaa, vitingoji na vijiji.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Bukombe ambae ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye maadhimisho ya Mwalimu Duniani wilayani Bukombe katika uwanja wa shule ya Sekondari Ushirombo.
Dkt. Biteko alisema wananchi ni muda wao wa kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 hali ambayo itawafanya kuchagua viongozi bora.
Pia Dkt. Biteko aliyasema hayo leo Oktoba 11, 2024 mara baada ya kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Kituo cha Kujiandikisha Mpiga Kura cha Shule ya Msingi kata ya Bulangwa.
“ Zoezi hili linaanza leo kama lilivyo zinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na zoezi hili litafanyika hadi Oktoba 20, 2024, hivyo nawaombeni Wananchi wa Bukombe mjitokeze ikiwa waandikishaji wamejiandaa vizuri na tunataka tuone orodha ya watu wote ili muda ukifika muweze kupiga kura walimu na wananchi tuhamasishaneni kujiandikisha,” alisema Dkt. Biteko.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella amempongeza Dkt. Biteko kwa kazi njema ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha na ya kuwaunganisha walimu hali ambayo imekuwa ikiifanya Bukombe kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la Saba, kidato cha nne na Sita huku Serikali ikiendelea Ku ajili walimu wa kada mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano Mwalwiba alisema Jimbo la Bukombe lina vituo 348 na mategemeo ni kuandikisha wananchi 109,124.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia walimu na wananchi katika maadhimisho hayo ya walimu Duniani Wilaya ya Bukombe alianza kwa kumpongeza Dkt. Biteko kwa kazi nizuri ya kuazisha siku ya Mwalimu Bukombe.
Waziri Mkuu Majaliwa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wa piga kura ili kuwa na ahadi ya kikatiba ya kupiga kura siku ya uchaguzi.
Majaliwa akizungumzia masilahi ya walimu kwa kuzingatia kauli mbiu ya walimu Duniani Wilaya ya Bukombe "Walimu ni Nyota Inayo Angaza" Alisema Serikali imefanya Mambo mazuri na makubwa kwenye Sekta ya Elimu ikiwemo sh 1.3 trioni zimelipwa kwa walimu waliopandishwa madaraja mapya na inaendelea na kuboresha kujenga miundo mbinu za shule na kutekeleza sera ya Elimu Bure.
"Serikali itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu hivyo maofisa utumishi naagiza kutatua changamoto za walimu yakiwemo madai, na kuwapandisha madaraja kwa wakati na Maafisa Elimu wa wafikie walimu kwenye maeneo ya kazi na kuwasikiliza ili kutatua changamoto zao sio kuwasubilia ofisini", alisema Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa amewaagiza wakurugenzi watendaji na maafisa Elimu nchini "hakikisheni mnawasikiliza Walimu" ili kuendelea kuboresha Sekta ya Elimu kuanzia chini hali ambayo italeta motisha kwa walimu.
Comments
Post a Comment