VIJANA CHANGAMKIENI FURUSA ZA MAFUNZO YA WAAMUZI WA MPIRA WA MIGUU

Na, Ernest Magashi, Geita

Vijana wengi Geita wametakiwa kuchagamkia furusa za mafunzo ya uwamuzi wa michezo wa mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya ajira ndogo ndogo ambazo ni sehemu ya kukuza uchumi wao.


Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoani Geita Salum Kulunge wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya wamuzi wa mpira wa miguu mjini Geita vijana walio shiriki 15 na kupata cheti cha pongezi kwa kupata mafunzo. 

Alisema ni wakati wa vijana kutafuta ajira na kukuza kipato Chao kwa kazi ya uamuzi kwa kuhudhuria mafunzo yanapotokea akifunga mafunzo hayo aliwaomba vijana kujitokeza kwenye mafunzo ya wamuzi yanapo pangwa kufanyika mkoani hapa. 


"Ajira hii ya uamuzi vijana wengi hawaijui faida zake hivyo vijana jitokezeni kwenye mafunzo yanapotokea ili kupata ajira ndogo ndogo ili kukuza uchumi wenu na ikumbukwe ni kazi ambayo inaitaji waminifu na kujituma kwa kuepuka rushwa na upendeleo kwenye michezo badala yake ni usimamizi wa haki kwa kufata madili na ", alisema Kulunge.  


Mwenyekiti wa kamti ya mashindano chama cha mpira wa miguu mkoani Geita Baraka Ramadhani aliwaomba wamuzi waliopata mafunzo ya sheria za kuchezesha mpira wa miguu kwenda kusimamia sheria. 


Ramadhani alisema watakapopata nafasi ya kuchezesha wafate sheria na kanuni walizo fundishwa kwenye mafunzo ya utimamu wa mwili kwa wamuzi huku wakikuza uchumi wao.


Alisema mafunzo hayo  yalianza Agost 30,2024  na kufungwa Septemba 1,2024 kupitia nafasi hiyo aliwapongeza wamuzi kwa kazi waliyoifanya kwa msimu wa 2023/2024 ambapo kamati ya mashindano iliwalipa kwa asilimia 100 kutokana na wamuzi kujituma na walifanya vizuri hata mwaka huu watafanya vizuri ligi daraja la tatu. 

 

Miongoni mwa wa shiriki wa mafunzo hayo Mecktrida Chiristopher alishukuru uongozi wa chama cha mpira wa miguu na wamuzi mkoa wa Geita kwa kutoa mafunzo hayo ikiwa vitu alivyo fundishwa atavizingatia kutenda haki anapokuwa amepangwa kuchezesha. 

Mtoa mada katika mafunzo hayo Geofrey Msakila amabe ni daraja la uamuzi ligi kuu aliwaomba wanafunzi hao kusimamia sheria kwa kuzingatia zilivyo fanyiwa marekebisho na mamlaka ya juu, na kwamba viongozi wa vilabu watoe Elimu kwa wachezaji ili kuodoa mkanganyiko wa usimamizi wa sheria za mpira kwa kudai wameonewa.

Comments