Na, mwandishi wetu Bukombe
Mwili wa kijana mmoja mwedesha boda boda mkazi wa kitongoji cha Mabago kijiji cha Nampalahala kata ya Busonzo wilayani Bukombe Mkoa wa Geita Juma Pamba anaedaiwa kuwa na umri wa miaka 27 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa porini huku pikipiki ikiwa haipo.
Akizungumzia tukio hilo Diwani wa kata ya Busonzo Nicholaus Safari Mayala alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Septemba 21,2024 kijijini hapo baada ya kuja watu wakijifanya abilia.
"niko mkoa Geita kwenye kikao ila taarifa nimezipata nizakweli kuwa kijana huyo amekutwa amekufa na mwili wake ukatelekezwa pori la Bihalamulo Kahama na walioteda tukio hilo wakatoweka na pikipiki ya kijana huyo", alisema diwani Safari.
Safari alifafanua kuwa kijana huyo ali kuwa amenunuliwa pikipiki mpya na kaka yake ili aendeshe boda boda jana mchana walija watu wanaume wawili wakijifanya niabilia akaondoka nao leo kijana ameonekana amepoteza maisha na viungo vya mwili vimeteganishwa.
Alisema wahalifu hao ambao hawajajulikana walifanya unyama huo na mwili wa kijana kuutelekeza kwenye hifadhi ya pori la akiba la Bihalamulo Kahama na mwiliwake kunyofolewa bazi ya viungo na kutelekezwa kisha kutoweka na pikipiki ya kijana huyo.
Diwani Safari alisema alipo pata taarifa hizo alitoa taarifa polisi na wanaedelea na taratibu za kipolisi.
Safari aliomba vyombo vya dola kukomesha vitendo hivi ambayo vinachafua viongozi wa chama na serikali.
Mwendesha boda boda Mabula Paul akizungumzia tukio hilo ameiomba Serikali kuingilia kati kuzibiti mauaji kwa waedesha boda boda.
"nivijana bado wanajitafuta wameajiri na watu kulipa kilasiko hawana chochote wana familia zinawategemea harafu wanauwawawa na wimbi la wahalifu ambalo kila sehemu ya mkoa tunasikia tunaomba mauaji yakomeshwe", alisema Paul.
Naye Daniel Mpina mwendesha boda boda mjini Ushirombo aliomba polisi kuwakamata wahusika ikiwa wiki iliyopita mjini Ushirombo mtaa wa Kilimahewa mwendesha boda boda amenyongwa hadi kufa wakachukuwa pikipiki yake ambayo alikuwa analipia kila siku.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Sofia Jongo alipotafutwa kuthibitisha matuko hayo na kuelezea hatua zilizo chikuliwa na polisi simu yake iliita bila kupokelewa.
Comments
Post a Comment