Na, Zena Seleman, Bukombe
Mkuu wa shule ya sekondari Ikuzi kata ya Runzewe Mashariki Wilayani Bukombe morning Geita Abdulmajdi Yusuph amewaagiza wanafunzi kufikisha salami diwani wa kata hiyo kwa mazuli anayo wafanyia wanafunzi.
Wito huo aliutoa wakati Anita shukrani kwa diwani wa kata ya Runzewe Mashariki Mery Nchiba baada ya kukabidhi Masada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ikuzi.
Yusuph alisema licha ya kushukuru diwani amekuwa akinitoa malizake kuwapa wanafunzi wa kike taulo na kuchagia chakula.
Alisema awali kutokuwepo taulo za kike walikuwa wanachagamoto sana lakini kwa saivi zitawasaidia sana kipindi wawapo shuleni.
"Nawaomba wanafunzi fikisheni salama za diwani na kusema kwa wazazi na walezi wenu Mambo mazuri anayofanya nimambo mazuri anatufanyia hapa shuleni nijambo la kuigwa na wengine", alisema Mwalimu Yusuph.
Akizungumza kwa niamba ya wanafunzi wa kike shule ya sekondari Ikuzi Anita Kalakwi alimshukuru diwani huyo kwa kuwa na moyo wa dhati wakujitoa kwa kuwapa taulo ili wapate elimu iliyo salama.
" tunakushukuru sana diwani wetu kwa kutushika mkono sisi kama wanafunzi tunaahidi tutajitahidi ili tuweze kusoma kwa bidii na kufaulu kwani hatuna changamoto ambazo zitatufanya tushindwe kuendelea na masomo hasa wakati wa hedhi", alisema Anita.
Diwani wa kata hiyo Mary Nchiba akikabidhi taulo hizo amewataka wanafunzi kuacha utoro haswa kwa wale wanaojikita kutafuta Pesa katika uchimbaji wa madini ambapo watawasababisha wazazi wao kukamatwa kwasababu ya utoro kutokufika shuleni.
Comments
Post a Comment