Na Abubakari Msita - Bukombe,Geita
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa geita (CCM) Mhe Rose Busiga Leo Tarehe Agosti 07.2024 Amefika hospital ya Wilaya ya Bukombe akiambatana na Baadhi ya Wajumbe wa UWT wilaya ya Bukombe na Kutoa Mahitaji kwenye wodi ya Wazazi pamoja na Wazazi waliojifungua.
Mbunge Rose Busiga ametoa Mashuka 20 kwaajili ya hospital na Mashuka 10 kwaajili ya kituo cha Afya msonga pia amegawa sabuni za unga pamoja na mche, kanga na mabeseni kwa wazazi waliojifungua tayari
Halikadharika Mbunge huyo amefurahishwa na Huduma zitolewazo katika hospital hiyo ya Wilaya na kuwapongeza kwani wanatumia kauli nzuri wawapo katika majukum ya kuwahudumia wananchi.
" Napenda kuwapongeza sana Watumishi wa idara ya afya kwani Mnahudumia Vizuri wananchi wetu na pia wananchi wanafurahia huduma hii ya afya ilioboreshwa na Mheshimiwa Rais Samia kwa kuweza kuongeza Majengo Likiwemo Jengo la dharula, Jengo la bima, chumba cha upasuaji na Madawa yanayoletwa na Mheshimiwa rais, pia tunampongeza mheshimiwa Dkt Biteko Ambae ni mbunge wetu na naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati kwa kupambana na kuweza kuleta za maendeleo kwatika wilaya yetu ya Bukombe" alisema Mbunge Rose Busiga.
Akizungumza Baada ya kupokea Vifaa hivyo Mganga Mkuu wa hospita ya Wilaya ya Bukombe Dkt Deograsia Mkapa amemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa kutoa kwani imewapa moyo watumishi wa hospital na Wazazi waliojifungua pia ameweza kuwahahikishia wananchi kuwa wataendelea kutoa huduma kwa usawa bila upendeleo wala kutikuwepo na kauli zisizo nzuri kwa wagonjwa kwani wameweza kujiwekea utaratibu mzuri wawapo katika mazingira ya kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Runzewe Mashariki Mary Nchiba Amepongeza juhudi za Rais samia kwa kusogeza huduma muhimu kwa wanachi kwani zimeweza kupunguza changamoto zao kwa kiasi kikubwa, pia amewataka Wananchi waendelee kumuombea Rais Samia afya njema ili azidi kuwatumikia wananchi wa Tanzania, pia kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Dkt Biteko ambae ni mbunge wa jimbo la Bukombe ili aweze kuendelea kuibadilisha Bukombe kwa kuipanmbania na kuweza kuleta fedha za miradi mbali mbali katika jimbo la Bukombe.
Comments
Post a Comment