BUTINZYA STAR YATINGA FAINALI KWA KUICHAPA 4-3 NAMONGE FC

Na, Ernest Magashi

Timu ya Butinzya fc imetinga nusu fainali baada ya kutoa kichapa gori 4-3 Namonge fc katika ligi ya KNK CUP meaka huu uwanja wa Namonge.

Magiri hayo kwa timu ya Butinzya fc yamepatika Nyumbani na ugenini ikiwa Namonge Star walienda katika uwanja wa Butinzya walikubali kupokea kichapo cha gori 3-2  na timu ya Namonge wakiwa Nyumbani Namonge fc walikubali kutoka sare ya 1-1.

Katika mchezo wa timu hizo mbili zikitimua vumbi katika uwanja wa Namonge timu ya Namonge star waliaza kwa kuifunga gori kupitia kwa Robart Simon Dakota ya 32 na kukubali kusawazishiwa na Butinzya kupitia kwa Swedy Kaguta Dakika ya 65.

Nahodha wa timu ya Namonge star Emmanuel John alisema mpira unamatokeo matatu kufungwa, kutofungwa, na kusare hivyo sisi timepoteza kwa kufungwa tunapambana kusaka mshindi wa tatu. 

Nahodha wa timu ya Butinzya fc Swedy Kaguta alisema wametumia nafasi wamefunga nahata mchezo wa kwanza walitimia nafasi na kuzifanyia kazi.

"Nawashukru wachezaji wezangu kwa ushirikiano waliouonuesha uwanjani na Mungu ametilinda tumepambana salama aendele kutulinda", alisema Kaguta. 

Mratibu wa mashindano ya Knk cup wilaya Busco Mwidad amesema siku ya fainali itatolewa baada ya kamati ya mashindano kukutana mapema na kwamba kabla ya fainali zitakutana timu ya Carpenter fc na timu ya Namonge star mchezo huo utaamua nani mshindi wa tatu kuelekea siku ya fainali kati ya Bugelenga na Butinzya.

Comments