WANANCHI ANZISHENI ULIINZI SHIRIKISHI KUDHIBITI VIBAKA KILA MTAA



Na, Ernest Magashi-Bukombe

Wananchi Wilayani Bukombe mkoani Geita wametakiwa kuanzisha ulinzi shirikishi kwenye mitaa yao ili kudhibiti makundi ya waharifu wakiwemo wanaowakatili watoto kwa kuwalawiti na kuwabaka. 

Wito huo umetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sofia Jongo wakati akihamasisha wazazi na walezi kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Jimbo la Bukombe katika uwanja wa mpira kata ya Lyambamgongo kukemea na kudhibiti tabia  mbaya nyumbani zinazoazishwa na watoto.

Kamanda Sofia alisema, wazazi na walezi hawana budi kulea watoto wao kwa kufuata utamaduni wa kiafirika na kuacha tabia za kuwaachaniza watoto wakuwe wanavyoona hali ambayo inakuwa inategeneza vibaka na watu wenye tabia mbaya mitaani. 

"Kutokana na kuzidi kuporomoka kwa maadili na kufuata utamaduni wa ki Tanzania watoto wa kike kuna makudi wanasagana, wengine vibaka ni hatari sana kwa taifa letu na waomba sana wazazi tuwafundishe watoto kuacha tabia hizo", alisema Kamanda Sofia. 

Kamanda Sofia akielezea mbinu za kudhibiti uhalifu ambao umekuwa ukifanywa na vibaka amewaomba viongozi wa mitaa kuazisha ulinzi shirikishi ili kupambana na vibaka kwa lengo la kushirikisha polisi wanapo kamata mhalifu na sio kujichukulia sheria mkononi.

Kupitia mkutano huo kamanda Sofia alikemea vikali wanawake kupiga waume zao huku akiwataka wanaume kuacha kuwafanyia ukatili watoto wa kike.

Alisema matukio ya aina hiyo yapo mkoani hapa na kwamba Serikali haita mwacha salama mtu atakae bainika kufanya ukatili wa kijinsia iwe kwa mtoto.

"hapa nawaomba wananchi kuendelea kupiga ukatili hasa akina baba imefikia sehemu ya kubaka watoto wao.

Mbunge wa jimbo la Bukombe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alisema jamii inatakiwa kubadilika kwa kukemea ukatili na kutegeneza jamii nzuri kwa kuwekeza kwenye Elimu.

Dkt. Biteko alisema Serikali inafanya mambo mazuri na mengine yanakuja ili kufikia malengo ya Serikali jiadikisheni kwenye daftari la wapiga kura ili mchaguwe viongozi bora na sio bora viongozi. 

Dkt. Biteko aliahidi kupambana ili kuipandisha hadhi zahanati la Lyambamgongo iwe kituo cha Afya ili wananchi wapate huduma za afya karibu. 

"kunawatu watakuja kuongea maneno ya ila waacheni wasene na msiludishe maneno mabaya  waonyesheni mabo mazuri yanayofanywa na Serikali zikiwemo Zahanati, vituo vya afya, na hospitali pamoja na shule", alisema Dkt. Biteko. 

Dkt. Biteko alisema mwaka huu tunauchaguzi wa Serikali za mtaa tusiuchukulie poa uchaguzi wananchi ambao mmefikia umri wa kupiga kura nendeni mkajiadikishe mirago itakuwa wazi Agost 5, 2024.

"uongozi ni mtu anaeweza kuwaweka pamoja watu anaowaongoza, nakwamba anaweza kujitokeza mgombea hana fedha ila nimzuri msimnyime kura mchagueni mschaguane kwa ukabila, dini, chagueni kiongozi atakae fanyakazi za maendeleo kwa misingi ya ilani ya chama cha mapinduzi. 

Awali diwani wa kata ya Lyambamgongo Boniphance Shitobelo alimshukru Mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt. Biteko kwa kuendelea kusukuma maendele huku Serikali ilileta fedha za miradi ya maendeleo.

Comments