Ameyasema hayo katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy Magani katika ziara yake ya kikazi katika kata ya Lyambamgongo Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
" nipende kuwaomba akina mama wenzangu kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji na uchaguzi mkuu 2024_2025 tujikite katika kupinga vitendo vya uvunjaji wa amani ili tuweze kupiga kura na kuchagua viongozi kwa Sheria taratibu na haki kwa kila mgombea." alisema Teddy
Hata hivyo Teddy owaomba wajumbe wa mkutano huo kuweza kumuunga mkono Rais Samia kuelekea katika uchaguzi mkuu kwa kumpa kura za kishindo Mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt. Doto Biteko kutokana na mambo mazuri ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa.
Kwa upande wake diwani viti maalumu tarafa ya Bukombe pili kondela ambae pia ni mlezi wa UWT kata ya Bukombe amewaomba wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wana muunga mkono Rais Samia kwa kumpa matunda katika uchaguzi mkuu ujao 2024_2025.
Awali Katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy mageni ametembelea nyumbani kwa mabarozi 7 waliopo katika kata hiyo ya lyambamgongo huku akihamasisha watu wajitokeze katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Comments
Post a Comment