- Get link
- X
- Other Apps
Na, Ernest Magashi-Bukombe
Wananchi wameaswa kutouchukulia poa uchaguzi wa Serikali za mtaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwaka huu.
Wito huo ulitolewa na Mbunge wa jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko wakati akihutubia mamia ya watu kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Ilyamchele kata ya Namonge akihamasisha wananchi kujiadikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wachaguwe viongozi bora.
Dkt. Biteko aliwaomba vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35 ambao hawamo kwenye daftari la wapiga kura nimudawao kuazia Agost 5,2024 kwenda kujiadikisha ili wawe na haki ya kupiga kura kwa kuchagua viongozi bora.
"Nendeni mkajiadikishe na tunaenda kuchagua, tusiagalie mwenywe uwezo anaweza akawepo mgonbea siowa kabila lako na wala dini yako kama anasifa za kuchaguliwa mchagueni", alisema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko aliwaomba wananchi mda ukifika wa kupiga kura wachague mwenywenia njema ya kuleta maendeleo na kuwaunganisha wananchi na si yo wa kuwagawa.
"Musichaguwe mtu kwasababu ananafasi ya kifedha badalayake chaguweni kiongozi wa kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo", alisema Dkt. Biteko.
Katibu Tawala Wilaya ya Bukombe Aly Mketo akimpongeza Mbunge kwenye mkutano huo alisema Wilaya inavijiji 64 vyote vinaumeme vitongoji 348 huku vitogoji 144 Vimepata umeme.
Mketo alisema Dkt. Biteko wakati anaigia Bungeni 2016 Wilaya ilikuwa na shule za sekondari 12 hadi sasa zimeongezeka hadi kufikia 26 kwenye kata 17 shule tatu zina kidato cha tano na Sita.
Alisema kuwepo kwa shule za kidato cha tano na Sita kimeondoa chagamoto ya wanafunzi kusafiri kwenda Mikoa jirani ambao walikuwa wanafaulu kwenda mbali kufata shule ya kidato cha tano na Sita wamekuwa wakisomea shule za Bukombe.
Diwani wa kata ya Namonge Mlalu Bundala alimpongeza Mbunge Dkt. Biteko kwa kuleta maendeleo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment