Na, Ernest Magashi-Bukombe
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewaagiza wa kuu wa Wilaya na wakuu wa mikoa nchini kuanza msako wa wanafunzi ambao hawajaripoti shule.
Agizo hilo alilitowa wakati wa ziara yake ya siku tatu jiomboni kwake Bukombe wakati akihutubia kwenye mikutano ya hadhara huku akiwaomba wazazi na walezi wapeleka watoto shule kabla ya kukamatwa.
Dkt. Biteko kwenye mkutano wa hadhara kata ya Namonge na kata ya Runzewe Magaribi na Lyambamgogo alisema kuna wazazi hawapeleki shule watoto kwamadai wanawasaidia kazi kitu ambacho hakitakiwi.
"Mkuu wa Wilaya ya hapa na Mkuu wa mkoa huu mnanisikia na wengine nchi nzima naagiza wanafunzi wote wafatiliwe na waende shule mzazi au mlezi atakae kwamisha wa kuu wa Wilaya na wakuu wa mikoa Serikali imchukulie hatua lengo mtoto aende shule", alisema Dkt. Biteko.
Aliongeza kuwa Serikali inalipa
ada kuanzia chekechea hadi kidato cha nne ikiwa niutekelezaji wa sera ya Elimu bure harafu kwa matakwa ya mzazi anataka asaidiwe kazi na mwanafunzi hapana.
Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteka akitoa ma agizo hayo kwa madc na marc Kuwasaka wanafunzi aliongeza kuwa kutompeleka mtoto shule inamkosesha haki zake za msingi za kupata Elimu hivyo lishugulikieni hili kwa ku unga jitihada za Ras Samia Elimu bure hakuna njia ya mkato ya kutowapeleka shule watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza kwenye mkutano wa Naibu Waziri Mkuu alisema maelekezo atayafanyia kazi.
Shigela alisema Serikali kwa mda mfupi imejenga shule 176 ikiwa nikuongeza madarasa kwa wanafunzi ambao inatakiwa waripoti shule hivyo wazazi wapelekeni shule watoto kabla ya kukamatwa.
Akizungumzia daftari la kudumu la wapiga kura Dkt. Biteko aliwaomba wananchi waliofikia umri wa miaka 18 kwenda kujiadikisha kuazia Agost 5, 2024 hadi Agost 11, 2024 ili wachaguwe viongozi wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu kwa kupiga kura.
Comments
Post a Comment