KATIBU WA UWT BUKOMBE AFIKA HOSPITALI YA WILAYA NA KUTOA POLE KWA BI REHEMA POUL ALIESHAMBULIWA NA KUKATWA KIGANJA CHA MKONO BUKOMBE
Katibu wa UWT wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Teddy Mageni Amefika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe kutoa pole kwa bi Rehema Poul ambaye amejeruhiwa na kupelekea kukatwa Kiganja kimoja cha mkono usiku wa kuamkia tarehe 25 Julai mwaka huu katika kitongoji cha kapela kaya ya Igulwa .
Aidha Teddy ameliomba jeshi la polisi pamoja na Serikali kuhakikisha linachukua hatua kali za kisheria dhidi ya watuhumiwa hao , huku akitoa wito kwa wananchi kulindana wao kwao ili uweza kuepusha matukio ya kikatili kama hayo.
Dada yake Rehema aliyejitambulisha kwa jina la Gaudensia George aliyekutwa wodini hapo akimuuguza ndugu yake pamoja na kupongeza jitihada za hospitali ya wilaya katika kunusuru maisha ya ndugu
Aidha, Mwenyekiti wa kitongoji cha Igulwa Kata ya Igulwa, Lucy Samweli alisema kuwa alipigiwa simu majira ya saa mbili za usiku na kuelezwa kuwa Rehema amekatwa na kitu chenye ncha kali ambapo alifika na kupiga simu polisi ambao walifika haraka na kumuwaisha hospitali ya wilaya.
“Kufuatia tukio hili la kusikitisha natoa wito wito kwa wananchi wangu tujilinde sisi kwa sisi” alisema Lucy na kuongeza kuwa mpaka sasa watu wane tayari wamekamatwa kufutia tukio hilo.
Jirani wa majeruhi, Joyce Selenda ameeleza kusikitishwa na tukio hilo kwa kuwa jirani yake Rehema wa kwa mama Esther alikuwa ni mtu aliyeishi vizuri na majirani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Sofia Jongo alipopigiwa simu kuthibitisha kutokea kwa matukio hayo
simu yake iliita bila majibu.
Wananchi waliozungumza na Bukombe sasa wamelitaka jeshi la polisi kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali watakaobainika kuhusika katika matukio hayo ya kikatili.
Comments
Post a Comment