Na zena Selemani, Bukombe
Ameyasema hayo katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy Mageni wakati wa ziara yake ya kuwapa semina ya uongozi makatibu wa UWT ngazi zote katika kata ya uyovu Wilayani Bukombe mkoani Geita.
,,sisi wanawake ni jeshi kubwa naimani tutafanya vyema katika uchaguzi mkuu wa Serikali za vijiji na vitongoji mwakaa huu naimani hatutamuangusha Rais Samia na mbunge wetu Dkt. Doto Biteko kwa sababu sisi wanawake tukiamua tunaweza."alisema Teddy
Hata hivyo Mageni waliwasihi wanawake wajitokeze katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji, na vitongoji na uchaguzi mkuu 2024_2025 kwaajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi .
Naye katibu wa UWT kata ya uyovu Mariamu Amri alisema jumuiya ya wanawake UWT imekuwa chachu ya maendeleo katika jamii kumekuwa na maendeleo mengi yaliofanywa kupitia jumuiya hii hata hivyo pia tunamshukuru sana Dkt Doto Biteko Mbunge wetu, Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati, amekuwa kiongozi mwema sana na ameleta maendeleo makubwa sana ikiwemo kunjenga, zahanati , shule, na vituo vya afya ndani ya wilaya yetu kwa ujumlaaa.
Comments
Post a Comment