Na, Ernest Magashi, Kahama
Timu ya Bukombe Combine sc imetinga nusu fainali baada ya kuifunga 3-1 timu ya Kagongwa fc katika mchezo wa ligi ya Gold fm kwenye uwanja wa Taifa wa Kahama.
Wafugaji wa magoli ya Bukombe Combine sc Dakika ya 15 Mtawala Magoti goli la pili Dakika ya 60 Visenti Buyenze na Dakika ya 87 Atony Mwalyoyo.
Mfungaji wa Kagongwa fc dakika ya 23 Abdallah Mapande.
Nohodha wa timu ya Bukombe Combine sc Ally Kasagula akizungumzia mchezo huo alianza kwa kumshukru Mungu na wachezaji wenzake kwa kujituma kwa kufuata maelekezo ya Mwalimu.
Kasagula alisema wamecheza kwa kila mmoja kuonyesha kipaji chake kwa kuipigania nembo ya KNK na wataendelea kujituma.
Nahodha wa timu ya Kagongwa fc Yasin Baroha alisema hawakutegemea matokeo hayo mabaya na kilichowatoke nikutokana na makosa waliyoyafanya uwanjani.
Baroha aliongeza kuwa timu ya Bukombe Combine sc ilikuja imejipanga na sisi tuliamini tutashinda lakini imekutofauti nisehemu ya mchezo tumekubari tumegongwa na kutoka kwenye mashidsno.
Comments
Post a Comment