Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko wakati akihutubia mkutano wa hadhara Kata ya Bugelenga wakati wa ziara yake ya kwenda anahamasisha maendeleo.
Dkt. Biteko amewaomba wananchi kuwekeza kwenye Elimu kwa kupeleka wanafunzi ambao bado wanasomeka watoro kidato cha kwanza mwaka huu.
" Nawaombeni wananchi wenzangu watu wema wa Bukombe sio vyema hadi Mkuu wa Mkoa wa Geita anze Kusaka wanafunzi ambao hawaja ripoti shule mwaka 2024 huku niwajibu wa mzazi kupeleka mtoto shule nawaombeni niwaelezeni kwenye Elimu kunamanufa makubwa",alisema Dkt. Biteko.
Alisema Rais Samia Suluhu Hasan ameleta fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo kujenga shule za sekondari na msingi lengo la Rais Samia nikuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Katika hatua nyingine akihamasisha maendeleo ametoa bati 135 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati na mifuko ya saruji 400 kwa ajili ukamirishaji wa miradi yote iliyokwama Kata nzima kwa kukosa saruji.
Diwani wa kata ya Bugelenga Donald Lubigisa alimshukru Mbunge kwa kuwaletea maendeleo na kutaja baadhi ya changamoto ambazo zilitatuliwa na Mbunge ikiwemo kutoa mabati na saruji.
Mkazi wa Bugelenga Sarah Faustin amisema Mbunge amekuwa msada Mkubwa kwenye maendeleo kila anapo fanya ziara anaacha alama kwa wananchi kwa kuchagia maendeleo.
Comments
Post a Comment