WANAWAKE TUJITOKEZE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA "BUKWIMBA"

 


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Geita Mhe. Lolesia Bukwimba amewataka wanawake mbalimbali wilayani Mbogwe Mkoani Geita kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Bukwimba ameyasema hayo leo Juni 25, 2024 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa UWT wilaya ya Mbogwe pamoja na Makundi mbalimbali ya wanawake wilayani wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya baraza la UWT Mkoa wa Geita amesema serikali inatoa fursa kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake katika utekelezaji wa Miradi pamoja na kuchangamkia Mikopo inayotolewa na serikali ili kuwawezesha kuwa na mitaji ambayo itawainua katika Biashara mbalimbali wanazozifanya katika vikundi vyao kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Bukwimba ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wakina Mama kuchangamkia kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa kwani wakina Mama wengi wamekuwa na hofu ya kugombea licha ya kuwa uwezo wakuongoza hivyo wanapaswa kushiri vyema kwa kuhakikisha wanachuka fomu katika nafasi ambazo wanaona wanaziweza kuhu akiwataka kuwahamasisha wanawake pamoja na wanawake kujiandikisha pindi mda utakapofika ili kuwa na sifa zaidi ya kupiga kura katika maeneo yao.

Aidha Katibu wa UWT Mkoa wa Geita Habiba Msimu wakati akizungumza na wanawake hao nae hakusita kuwakumbusha jukumu la kugombea pamoja na kuwataka kuhakikisha wanamchagua Mwanamke imara katika nafasi hizo za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha wanachagua viogoI imara na wachapa kazi.

Naye Mjumbe wa baraza kuu Taifa Merry Mazula  ametumia nafasi hiyo kuwasihi wakina Mama pale ambapo wanafanikiwa kujikwamua kiuchumi kupitia pesa wanazokopeshwa na serikali kuacha tabia ya  kuwazarau  waume zao na badala yake washirikiane nao katika kuendeleza mafanikio ya Familia.

Nao Baadhi ya viongozi na wanawake katika makundi mbalimbali waliofika katika Mkutano huo wamemshukuri Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Mhe. Lolesia Bukwimba  kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kuwafikia katika maeneo yao na kuwahamasisha katika kuchamkia furasa pamoja na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa ujao kwani kwao imekuwa fursa kubwa ya kuwakumbusha nakuwafanya kuwa tayari katika kuchangamkia fursa hizo.

Comments