WANANCHI CHAGUENI VIONGOZI BORA SERIKALI ZA MITAA

 

Wananchi wilaya ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kutumia kadi za kipigia kura vizuri katika uchaguzi wa Serikali za mtaa utakao fanyika Oktoba mwaka huu. 

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Katome wakati akihamasisha wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuhakiki taarifa zao. 

Dkt. Biteko aliwaomba wananchi kutumia hakizao za msingi kwa kubiga kura na kuchavua viongozi bora na sio bora viongozi. 

"Nawaomba wananchi mjue kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za mtaa hivyo wakati wa kuhakiki daftari la wapiga kura ukifika nendeni mkaadikishwe ili mwenasifa za kupiga kura na mwezi Oktoba 2024 pigeni kura kwa kuchagua viongozi bora ambao watawaleteeni maedeleo kwa gazi ya kitongoji na vijiji, mtaa", alisema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko aliongeza kuwa kwa wilaya ya Bukombe kupitia uchaguzi wa Serikali za mtaa tumlipe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchagua viongozi kupitia CCM kwa makubwa ambayo amekuwa akifanya kwa kuwaletea fedha nyingi za miradi ya maendeleo. 

Hata hivyo kupitia mkutano huo Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko amewataka watendaji wote wa Serikali nchini kuwafuata wananchi kusikiliza shida na kutatua kero zao 

Diwani wa kata ya Katome Joseph Maganga alimshukuru Mbunge wa jimbo la Bukombe kwa kuendelea kuisukuma Serikali kuleta fedha za miradi ya maendeleo haliambayo wananchi wanafurahia Serikali yao.

Mbunge viti maalumu mkoani Geita Rose Businga alisema wananchi wa Bukombe kwa maendeleo ambayo yanaletwa na Serikali wananchi waendelee kumuunga mkono Mbunge na kuhakikisha Rais Samia wanamuombea kwa Mungu ili achapekazi kwa lengo la kuwaletea fedha kwa tanzania.

Comments