SHDEPHA KUANZA KUFANYA UTAFITI WA STADI ZA MAISHA KWA WATOTO NA VIJANA 375 BUKOMBE

 


Na, Ernest Magashi-Bukombe

Tasisi isiyo ya kiserikali Wilayani Bukombe mkoani Geita inayo jishughulisha na mambo ya kijamii SHDEPHA + BUKOMBE imeanza kufanya utafiti kwa vijana 375 majumbani kwa ajili ya sitadi za maisha.

Akizungumza kwenye semina ya siku tatu ya kuwapatia mafunzo vijana 32 ambao walikizi vigezo kwenye tasisi ya SHDEPHA  kwa ajili kwenda kufanya utafiti kwa watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17.

Mratibu wa SHDEPHA BUKOMBE Esau Malifedha ameongeza kuwa mradi huu umepangwa kufanyika katika kata   (14) na kaya (375) zilizopo kwenye vitongoji 25 Wilayani humo

" Mafunzo hayo ni manzuri na nitahakikisha nachukua takwimu ya watoto kuhusu stadi za maisha kwa Uhakika ili kila mmoja aweze kufikiwa na mpango huu,"alisema Jacqueline Ernest. 

Afisa mipango Mwandamizi Samson Sitta ameitaka jamii kuwa na ushirikiano kwa vijana walipewa  mafunzo hayo ili kuwafikia vijana kwenye kaya zilizo kwenye mpango. 

Mwenyekiti wa SHDEPHA + BUKOMBE  Esther Gwanko ametoa shukrani kwa mashirika ambayo yamekuwa yakishirikiana na Shdepha kwa kutekeleza miradi kwenye jamii ikiwemo ya utoaji Elimu.

"Lengo na madhuni ni kupima katika stadi za maisha na maadili katika wilaya yetu ilikuwa chini katika hali ya kujitambua na katika suala la utatuzi wa watoto  walikuwa chini hata katika maadili ilikuwa chini, " Alisema Esther. 

Awali Kaimu Mkurugenzi mtendeji wa halmashauri ya Bukombe Sida Shalali akifungua mafunzo hayo aliwaasa vijana kwenda kufanya kazi kwa usahihi ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa na tasisi hiyo.

Comments