MWENYEKITI UWT MKOA WA GEITA AFIKA MSIBANI KUTOA POLE KWA DIWANI VITI MAALUMU CHATO JENISTA GABRIEL ALIEFIWA NA MME WAKE.
Na zena seleman
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Geita Lolesia Bukwimba akiambatana na Katibu wa UWT Mkoa wa Geita Habiba Msimu na Mjumbe wa baraza kuu Taifa Merry Mazula leo Juni 25, 2024 wamefika kutoa salam za pole nyumbani kwa diwani wa viti maalu tarafa ya kachwamba wilaya ya Chato Mkoani Geita Jenista Gabriel alieondokewa na Mme wake.
Msiba huo ulitokea usiku wa kuamkia juni 24, 2024 wakati Mme wa Diwani huyo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa wilaya ya Chato Mkoani Geita ambapo Marehemu atazikwa katika kijiji cha ImalaBupina kata ichwankima wilayani humo.
Mhe. Lolesia kwa Niaba ya Umoja wa Wanawake Wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Geita amesikitishwa na kifo hicho nakutoa pole kwa niaba ya wanawake wa umoja huo huku akimuomba Mhe. Diwani Jenista Gabriel kuwa mvumilivu na kumtegemea Mungu katika kipindi hiki kigumu na chama cha Mapinduzi CCM kitakuwa na familia hiyo katika kipindi chote.
Aidha Mhe. Lolesia amewataka viongozi mbalimbali wa UWT katika Mkoa wa Geita kuwa na utaratibu wa kufarijiana kwenye vipindi vyote vya furaha na huzuni kwani wote ni wamoja na wnapaswa kupendana katika kila hali.
Comments
Post a Comment