Madiwani Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na Mabalozi kushirikiana ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko wakati akihutubia kwenye kikao cha mabalozi zaid ya 720 kutika kata 17 kwenye viwanja vya ofisi ya CCM wilaya.
"Tangu CCM kuanza mabalozi ndio viongozi wa mashina na kwamba nisehemu ya viongozi wa chama hivyo wanatakiwa kuijua na kuisemea miradi ambayo inasimamiwa na madiwani", alisema Dkt. Biteko.
Matondo Lutonja alimshukru Mbunge kwa kuwaunganisha mabalozi na Madiwani na kwamba kupitia kikao hicho CCM Wilaya na mkoa walimpongeza Mbunge kwa kazi anazofanya kwa mahusiano mazuri na viongozi kuanza mabalozi.
Akizungumza kwa niamba ya mabalozi wa shina Ng'anzo Rosemere Mabunga alisema amefurahishwa na kitendo cha Mbunge kuwaita mabalozi ambao w amekuwa wakijiona wanyonge lakini kituita nakutukutanisha niupendo waketu.
Mabuga alisema licha ya upendo wa Mbunge kwa kila mtu amekuwa na ushirikiano mkubwa na Madiwani na maendeleo tunayaona sekta ya Elimu na Afya, na barabara zinajengwa.
Comments
Post a Comment