HALMASHAURI YA MBOGWE YA PONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

 


Na, Ernest Magashi-Mbogwe

Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita imepongezwa kwa kupata hati safi kutokana na uajibikaji mzuri wa madiwani na watalamu ikiwemo kujibu hoja za CAG. 

Pongezi hiso zimetolewa na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali mkoa wa Geita  Richson Elias na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martne Shigela kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani cha mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mjibu wa taarifa ya kuishia Juni 30, 2023.

Akitoa pongezi hizo Elias alisema halmashauri ya Mbogwe ilipokea mapendekezo ya hoja za miaka ya nyuma kuanzia 2014/20215 hadi 2021/2023 kuazia mwaka huo halmashauri ilikuwa na jumla ya hoja 77 hoja 47 ni zamiaka ya nyuma huku hoja 31 za mwaka wa ukaguzi 202/2023.

Elias alisema halmashauri ilifanyia kazi mapendekezo ya mkaguzi na kufanikiwa kufunga hoja 40 na kusalia hoja 37 ambazo zinatafutiwa majibu haliambayo ili ifanya halmashauri kupata hati safi kwa mwaka huu wa fedha. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela aliwapongeza madiwani na watalamu wa halmashauri hiyo kwa kupata hati safi huku akiwataka kuendelea na ushirikiano wa kuodoa hoja zilizobaki na kukusanya mapato ya ndani licha halmashauri imefikia asilimia 85 ya makusanyo. 

"Niwapongeze sana madiwani na watalamu kwa kupambana kujibu hoja na kuzifunga hadi kupata hati safi naombeni sana muendelee na ushirikiano ili kufikia malengo ya Serikali ifikapo Juni 30,2024" alisema Shigela. 

Akipokea pongezi hizo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Saada Mwalukwa alisema watafanyia kazi maelekezo ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Mkoa. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbogwe Visent Businga aliomba Serikali kuwaletea fedha ambazo wameomba ili kufikia malengo ya halmashauri kwa mwaka wa fedha utakao anza Julai 1, 2024/2025 haliambayo itawafanya kukamilisha miradi ya maendeleo likiwemo jengo la makao makuu ya halmashauri.

Comments