ASKOFU MKUU KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA AWATAKA WAKRISTO KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAKE
Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania Eliaza Issaka amewataka wakrsto kuendelea kumuombea Rais Samia na wasaidizi wake ili Mungu awalinde waendelee kuwatumikia wa Tanzania kwa kuwaletea maendeleo.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la wanawake wa kanisa la Pentekoste Tanzania llilofanyika Runzewe mashariki wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Askifu Issaka aliwaomba waumini kuendelea kutendamema kwa kuiunga mkono Serikali kwa kuielezea mazuri inayofanya.
" Nakuomba M/K wa UWT Mkoa wa Geita utufikishie salamu kwa Rais Samia asiwe na wasiwasi kabisa achapekazi na uchaguzi ukifika achukuwe fomu sisi kama ma Askafu tukishapitisha hakuna atakae pinga alisema Issack".
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Geita Lolesia Bukwimba amewataka wanawake kujitokeza katika uchaguzi mkuu na uchaguzi wa Serikali za vitongoji kwa kugombea nafasi mbalimbali huku akiwataka wamuombee Rais Samia kutokana na kazi nzuri anazozifanya
" niwaombe wanawake wezangu tujitahidi kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu na uchaguzi wa Serikali za vijiji na vitongoji kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia, "alisema Bukwimba.
Katibu wa umoja huo wa wanawake wa pentekoste Tanzania Estar Emmanuel akisoma taarifa alisema kongamono hilo tangu limeanza lina miaka 10 na limenufaisha wanawake wengi ikiwemo kujikita katika maombi na kuwafanya wakina mama wengi kuwa na malezi bora katika familia zao.
Alisema kongamano hilo litakuwa ndani ya siku sita ikiwa lengo ni kufundisha wanawake malezi bora na kujikita katika maombi ya kiroho ikiwemo kuiombea Serikali.
Comments
Post a Comment