WATENDAJI WA KATA MBOGWE WANAO ZIKATAA POS KUKIONA CHA MOTO


 Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe Sada Mwalukwa ametoa agizo ifikapo siku ya ijumaa tarehe 17-5-2024 watendaji wote wawe wamechukua posi zote 23 kwaajili ya kuanza kukusanya mapato kwaajili ya kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Agizo Hilo limetolewa wakati wa kikao Cha kawaida Cha robo tatu Cha Baraza la madiwani Cha  kusikiliza maendeleo ya kila kata na kutatua changamoto zake .

 "ifikapo siku ya ijumaa watendaji wote mchukuwe posi na atakae kataa niletewe taarifa ili hatua zingine za kisheria  zichukuliwe"alisema Mwalukwa. 


Mkuu wa Wiliya ya Mbogwe Sakina Mohamed aliiunga mkono agizo la mkurugenzi wa halmashauri hiyo na kuwataka watendaji kuacha uzembe na wafanye kazi ili kuisaidia wiliya kukua kiuchumi 

" haiwezekni kila siku tatizo liwe ni ukusanyaji wa mapato ifike hatua hili swala liishe na msipende kumlaumu afisa mapato wa wilaya kwa sababu anafanya kazi kubwa Sana mchana na Usiku Ila shida ipo kwa watendaji wetu wa kata wanakataa kuchukua posi kwaajili ya kukusanya Mapato wakati swala la ukusanyaji wa mapato linahusisha watumishi wote wa serikali" .alisema sakina

Kwa upande wake makamu  mwenyekiti wa  halmashauri ya Mbogwe Nsika Sizya amewashukuru mkurugenzi na mkuu wa wilaya ya Mbogwe kwa kutoa maagizo hayo kwani imekuwa ni kero sana kila siku kilio Cha madiwani imekuwa ni posi na ukusanyaji hafifu wa mapato na kupelekea wilaya kushuka kiuchumi. 


Comments