Viziwi wamshukuru Dkt. Biteko kwenye noti




Naibu Waziri, Mwanaidi afungua mafunzo Bukombe
BoT: Elimu imesaidia kupunguza tatizo la noti bandia

Na Henry Evarist, Bukombe.

Taasisi ya Maendeleo Kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) imempongeza Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko kwa kuwaongoza katika fursa mbalimbali za kushika noti kupitia biashara ya madini walemavu viziwi wa jimbo la Bukombe mkoani Geita.

Pongezi hizo zimetolewa Ijumaa Mei 10, 2024 katika ukumbi wa halmashuri ya wilya ya Bukombe wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya utambuzi wa noti yaliyoendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika wilaya ya Bukombe

Mafunzo hayo yaliudhuriwa na walemavu viziwi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, viongozi wa halmashauri wakiongozwa na mwenyekiti, Mohamed Yusuph, wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri, mkuu wa wilaya (aliwakilishwa na katibu tawala), kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wa CCM mwenyekiti na katibu wa wilaya.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi, viziwi walimpongeza mbunge wao Dkt. Biteko kwa kuwa stari wa mbele katika kutetea maslahi na ustawi wa makundi maalumu katika jimbo hilo ikiwemo fursa za elimu, matibabu na usawa kwenye ajira
Afisa Elimu Maalumu wilaya ya Bukombe, Joyce Mangi akisoma risala kwa mgeni rasmi

“Shukrani za pekee zimuendee Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko kwa kuendelea kusimama nasi bega kwa bega katika kusongesha gurudumu la maendeleo kwa jamii ya walemavu viziwi. Tangu awali amekuwa nasi kama mlezi wetu kwa kutushauri na kutusimamia pale tulipohitaji msaada wake” alisikika msoma risala, Mwl. Joyce Mangi

Mtendaji Mkuu TAMAVITA, Kelvin Nyema aliielezea wilaya ya Bukombe kuwa ina Viziwi wengi ambao hawana ufahamu kuhusu fedha na kuwa mwamko bado ni mdogo kwa jamii hiyo na kuishukuru benki kuu pamoja na serikali kukubali kufanyika kwa mafunzo hayo wilayani Bukombe na kumshukuru pia mbunge wa jimbo hilo kwa mchango wake katika kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyika.
Mtendaji Mkuu wa TAMAVITA, Kelvin Nyema akizungumza na Bukombesasa blogspot
Nyema alisema lengo la mafunzo hayo ni kudhibiti matumizi ya fedha bandia kwa sababu wamejitokeza watu wasioo wema kwa siku za hivi karibuni wakichapisha na kusambaza fedha bandia na viziwi kuwa miongoni wa waathirika wa utapeli huo na tamaa ya baadhi kutaka kujitajirisha kupitia madhaifu yao na hivyo mafunzo kuwasaidia kuepuka mtego huo wakiwemo wajanja kutambua fedha halali na zisizo halali

Aidha, mwakilishi kutoka Benk Kuu Kanda ya Mwanza, Restituta Minja mbali na kumpongeza mchango wa Dkt. Biteko kwa watu wenye ulemmavu katika Kanda ya Ziwa, alifurahishwa na jinsi jamii hiyo ya viziwi inavyoshiriki kikamilifu katika biashara ya madini wilayani Bukombe.
Mwakilishi wa Benk Kuu Kanda ya Mwanza, Resituta Minja akifafanua umuhimu wa mafunzo
Restituta aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kufadhili mafunzo ya utambuzi wa noti kwa makundi mbalimbali wakiwemo jamii ya wasioona, wabunge na wafanya biashara ili kupunguza uwepo wa noti bandia nchini.

Taasisi ya Maendeleo Kwa Viziwi Tanzania (TAMAVITA) ina wanachama 120 katika wilaya ya Bukombe ambapo kati yao ni wanume 55 na wanawake 65. 

Katika hotuba yake, Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaid Ali Khamis alieleza mkakati wa serikali katika kukwamua makundi yenye uhitaji maalumu wakiwemo wanawake, vijana na walemavu kupitia urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10 ya bajeti ya halmashauri.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu, Mwanaidi Ali Khamis akifungua mafunzo ya utambuzi wa noti kwa walemavu viziwi wilaya ya Bukombe Mei 10, 2024
Mwanaidi, aliwaagiza maafisa maendeleo ya jamii kote nchini kuacha kukaa ofisini na kwenda vijijini kukutana makundi maalumu yanayolengwa na serikali katika mikopo hiyo na kuwapatia elimu na kuhakikisha inawanufahisha


Maafisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Bukombe kwenye Picha ya pamoja na Naibu Waziri Mwanaidi Khamis
“Mheshimiwa rais ameelekeza mikopo hiyo ianze kutolewa katika mwaka wa fedha 2024/2025. Wananchi tumieni fursa hizi ili muweze kujkomboa kimaisha” alisema na kuziagiza halmashari zote nchini kutoa taarifa sahihi juu ya mikopo hiyo ya asilimia 10” alisisitiza Naibu Waziri, Mwanaid

Mshiriki wa mafunzo, Saliwa Revocatus kutoka Ushirombo aliishukuru benki kuu ya Tanzania kwa mafunzo hayo ya utambuzi wa noti akieleza kuwa yatawasaidia kuweza kubaini fedha halali na bandia.
Mshiriki wa mafunzo, Saliwa Revocatus
Saliwa aliiomba serikali kuwawezesha waliopata mafunzo kufika vijijini ili kufikisha elimu ya utambuzi wa noti kwa walemavu.

Paschal Elias ni mfanyakazi wa kampuni ya uchimbaji wa madini STAMICO na mkazi wa Bukombe anayeona mafunzo ya noti ni muhimu kwa jamii ya viziwi kutokana na ukubwa wa kundi hilo ambalo limeachwa mtaani bila utambuzi wa noti halali.
Paschal Elias
Elias alisema kutokana na mafunzo hayo na kwa kutambua kuwa viziwi wapo wengi vijijini wasio na utambuzi wa noti halali na bandia, anajitolea kutenga muda wake baada ya kazi kutembelea jamii hiyo na kuwapatia elimu aliyoivuna kutoka BoT.

Kuhusu ulinzi na usalama kwa watu wenye walemavu, Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Mhandisi Paskas Mulagiri aliwatoa taarifa kuwa hali ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bukombe ni shwari. 
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bukombe kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Mwanaidi Khamis wakati wa mafunzo ya utambuzi wa noti Mei 10,2024
“Hii imetokana na Jeshi la Polisi kujipanga kukabiliana na hali hiyo pamoja na kushirikisha wananchi katika suala zima la Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi” alisema

Katika kumarisha ulinzi, Wilaya ya Bukombe ina vituo vikubwa viwili (2) vya Polisi ambavyo ni Ushirombo na Runzewe. Pia vipo vituo vingine vidogo vitatu (3) ambavyo ni Namonge, Bukombe na Bulega. Vito hivi vidogo vitatu vimejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Serikali ili kumarisha Ulinzi katika maeneo hayo ambayo hayakuwa na vituo vya polisi kabisa.

Mulagiri aliyataja maeneo ya utawala ya wilaya ya Bukombe yenye wakazi 407,102 kuwa ni pamoja na tarafa tatu, kata 17 vijiji 64 na vitongoji 348 kati yake 20 ni vya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ushirombo. 

Katika mafunzo hayo ya utambuzi wa noti, viziwi wamemtaja sana mbunge wao wa sasa kuwa nyuma ya utulivu wa kisiasa na mshikamano wa makundi yote ya kijamii katika wilaya Bukombe ambapo bila kujali hali zao kila mmoja amehamasika kufanyakazi na noti kuzishika. 

Dkt. Doto Biteko

Comments