UWT YAPIGA MARUFUKU WAGOMBEA KUJINADI NA KUTOA VITU KWA WAPIGA KURA KABLA YA MUDA WA KAMPENI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SERIKALI ZA VIJIJI NA VITONGOJI 2024
Na Zena seleman
Ameyasema hayo katibu wa uwt wilaya ya Bukombe Teddy Mageni wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya utekelezaji wilaya ya kuhamasisha na kukagua uhai wa chama na jumuiya ya uwt katika kata ya igulwa wilaya Bukombe Mkoani Geita.
" Nimarufuku wagombea mnaotarajia kuchukua fomu za kugombea uongozi wa wenyeviti wa serikali za vijiji na vitongoji kufanya kampeni na kugawa vitu vikiwemo kanga, chumi, na vitu kwaajili ya kutafuta kura ukibainika hatutakuacha salama"alisema Teddy
Akisoma taarifa ya kata ya Igulwa kefleni Edson alisema hali ya kisiasa ipo shwari na tayari wanawake wengi wamejitokeza na kuchukua kadi za jumuiya ya uwt na kusajiliwa Katika mfumo wa kieletroniki
Na hivyo wanataraji Mambo mazuri na hawatamuangusha mhe Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa serikali za vijiji na vitongoji .
Diwani wa kata ya Igulwa Simon Mabenga kwa niaba ya wajumbe aliwashukuru kamati ya jumuiya ya uwt wilaya ya utekelezaji kwa kuendelea kuhamasisha na kukagua uhai wa chama na jumuiya ya uwt .
MWISHO
Comments
Post a Comment