Na, Zena Seleman- Bukombe
Viongozi wa matawi hadi kata Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamefundwa Mambo mbalimbali likiwemo la kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.
Semina hiyo ya kuwafunda imetolewa na Katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy Mageni baada ya kukagua uhai wa chama na jumuiya zake katika kata ya Bulega.
Teddy amewataka viongozi wa kata kutoa Ushirikiano kwa viongozi wa matawi na kuwaelekeza jinsi ya kufanya vikao na kuandaa miongozo ya vikao
"nipende kuwaagiza viongozi wa jumuiya ya UWT kila kata mshuke katika matawi yenu kwaajili ya kufanya vikao vyakazi ikiwa lengo nikuongeza wanachama wengi wa jumuiya ya UWT pamoja na wanachama wa chama Cha mapinduzi CCM"alisema Teddy.
Awali akisoma taarifa katibu wa UWT kata ya Bulega Kalekwa Methew alisema mpango wa jumuiya ya UWT katika kata yao nikuhakikisha wanawake wengi wanajitokeza na kuchukua fomu katika uchaguzi wa Serikali za vitongoji na Vijiji unaotaraji kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
"sisi viongozi tunaahidi kuelekea kuongeza wanachama wapya na kuwashawishi wanawake kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za mtaa hivyo tunamshukuru Sana Katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe kwa Kutufunda tunaahidi aliyoyaelekeza tutaifanyia kazi ", alisema Kalekwa.
Diwani wa kata ya Bulega Erick Kagoma ameishukuru kamati ya utekelezaji ya UWT Wilaya ya Bukombe kwa kuendelea kutoa Semina ya uongozi na pia amemshukuru sana Mbunge w Jimbo la Bukombe Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko kwa kuendelea kuleta maendelo katika Wilaya ya Bukombe ikiwemo kujenga shule za kisasa, zahanati mpya karibia kila kata na ameahidi kuendelea kuwa unga mkono wanawake wa UWT kila kata.
Comments
Post a Comment