UWT BUKOMBE YAWAPONGEZA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KUELEKEA KATIKA MITIHANI YAO INAYOTARAJIA KUANZA 6/5/2024


Na Jonathan Mgaya

UWT BUKOMBE  YAWAPONGEZA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KUELEKEA KATIKA MITIHANI YAO INAYOTARAJIA KUANZA 6/5/2024

Kamati ya Utekelezaji ya Uwt Wilaya ya Bukombe inayoongozwa na Mwenyekiti wake Juliet Simon wamefaya ziara ya kukagua uhai wa Jumuiya hiyo na Chama cha Mapinduzi kwa Ujumla kwenye Kata ya Bukombe na kutoa pongezi kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Akitoa Pongezi hızı Mwenyekiti Simon alisema ili Shule ya Sekondari ya Bukombe iendelee kufanya vizuri katika masomo lazıma Wazazi na Walimu washirikiane katika malezi ili kukinusuru kizazi kilichoko shuleni hapo

 “Sisi Kama wazazi furaha yetu  ni ,kuona watoto wetu wanafanikiwa kwenda mbali zaidi hivyo niwatakie mitihani mema wanafunzi wa kidato Cha sita mnaotarajia kuanza tarehe 6/5/2024”alisema Juliet.

Nae Katibu wa UWT Wilaya ya Bukombe Teddy Mageni aliunga mkono hoja ya Mwenyekiti kwa kuwaasa wanafunzia hao wasome kwa bidii na kuendelea kuiheshimisha Bukombe Kama ilivyo katika kila mwaka ambapo Bukombe imekuwa ikiongoza kimkoa katika upande wa sekta ya elimu.“aliseama Teddy


kia mitihani mema vijana wetu tunawaombea sana muweze kufauru kwani furaha ya wanabukombe nikuona watoto wao wanaufauru  mzuri nakuzidi kusonga mbele kutokana na miundombinu ya elimu ipo vizuri hivyo Basi nawaomba Sana msituangushe sisi wazazi wenu “alisema teddy

Comments